Wasaka hifadhi kwa Kilango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasaka hifadhi kwa Kilango

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  08 December 2009
  Na Yusuph Mussa
  Same, KILIMANJARO


  BAADHI ya wananchi wa Kijiji cha Goha, Kata ya Myamba wilayani Same, Kilimanjaro, wamekimbilia katika nyumba aliyofikia Mbunge wa Same Mashariki Bi. Anne Kilango Malecela wakiamini watakuwa salama, baada ya kunyesha mvua kubwa usiku wa kuamkia jana.

  Kitendo cha mvua hiyo kuwahamisha watu katika nyumba zao na kwenda alipofikia mbunge wao kijijini hapo aliyefika kwa nia ya kutoa msaada wa fedha na vitu mbalimbali, kilimweka roho juu Bi. Kilango kwa kuhofia maisha yake, huku akipiga simu kila mahali kuomba msaada wa kufanyiwa uchunguzi haraka kama milima hiyo ni salama ama la.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, baadhi ya wananchi walisema mvua hiyo ni mwendelezo wa nyingine iliyonyesha usiku wa kumkia Desemba 5, lakini hiyo haikuwa kubwa kama hiyo iliyonyesha usiku wa kuamkia jana, na kusema sasa hivi hawana amani mvua inaponyesha.

  "Sasa hivi hatuna amani mvua inaponyesha, kwa kweli tunaombea isinyeshe kabisa, kwani inaponyesha tupo tayari tunyeshewe sababu tunatoka nje kuona kutatokea nini, lakini sasa hivi hakuna mtu anapata usingizi akisikia mvua inanyesha usiku" alisema Bi. Naetwa Nkulu (80).

  Bi. Kilango alimtaka Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda kuharakisha wataalamu watakaoenda kuchunguza kwa kina miamba kama ipo salama kwa watu kuishi, kwani kati ya kata 14 za jimbo lake 10 zipo milimani, hivyo kutishia maisha ya watu.  nyamayao nyingine hiyo tena
   
Loading...