Wasaini mikataba kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasaini mikataba kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini......

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Smiles, Sep 2, 2010.

 1. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "Mambo ya SERIKALI hayo.....hehehe inafurahisha sana! kumbe hela tunazo eeh"


  Na Boniface Meena

  Kampuni nne za miradi ya kuchimba madini zimefanikiwa kupata mkopo kutoka SERIKALINI kupitia mfuko wa kuendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini.

  Kampuni zilizofanikiwa kupata mikopo hiyo ni: TAN Discovery Mineral Consultancy Ltd, Kilimo and General Supplies Co. Ltd, C. E Holdings Ltd na Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo wakati wa kutiliana saini jana za mikataba ya kupewa mikopo, alisema Sh milioni 650 zitatolewa kama mkopo wa riba nafuu kwa makampuni hayo.

  Alisema kampuni ya C. E Holdings wataanzania kituocha kuongeza thamani ya madini katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam na kampuni ya Kilimo and General Supplies watakuwa na kituo cha kukodisha vifaa katika eneo la Pongwe Musungura wilayani Bagamoyo.

  "Serikali itaendelea kutoa mikopo kwa makampuni na vikundi vingine vitakavyokuwa vinaendeleza miradi ya uchimbaji mdogo, vile vile itaendelea kutekeleza programu ya kuwakopesha wachimbaji wadogo" alisema Jairo.


  Source: Mwananchi
   
Loading...