Wasaidizi wa Rais Magufuli tafadhali jitahidini kumweleza kipi cha kusema na cha kutokisema kwani anajichanganya mno!

mkuu.... je, wewe ni binamu yake na yule GENTAMYCIN nini?
 
Mtoa mada ambacho hujakigundua ni kwamba, kati ya hiyo miaka 10 uliyoigundua; Miaka 5 ya mwanzo, mzee alikuwa kwenye kundi hatari la mashetani kama wenzake!

Na kwenye ile miaka 5 ya mwisho (mpaka muda huu tunaongea), alibadilika ghafla kwa nguvu za kimiujiza, kutoka kwenye lile kundi la mashetani na kugeuka kuwa Malaika mtakatifu na asiye na dhambi.

Yeye sasa ni wa kuabudiwa tu na kutukuzwa! Hivyo ana haki zote za kuwakosoa wale mashetani aliowaacha miaka ile 5 ya mwanzo kati ya hiyo 10.
 
Kwa hilo nakupinga
Hotuba sio Ngonjera
Trump anatumia Twitter na ulimwengu umemwelewa
acha awatumbulie hapohapo Jukwaani
kwa style hiyo inatufanya tusogee kwenye Luninga
sio km zile Hotuba za zamani za J Makamba wapinzani milikuwa mnazipata mapema mnarushiana kwenye mitandao
Kabla haijasomwa mnaanza kutoka Ukumbini
MBONA SASA HATUSIKII DHAIFU
 
Hujaelewa. Ye amewaambia tanroads kwa sasa hawana sababu ya kupanga sababu majengo mengi ya serikali yana nafasi baada ya serikali kuhamia dodoma. Yawezekana kipindi ye alipokuwa waziri haikuwepo hiyo nafasi pia hakuwa na meno kama aliyonayo sasa ya kuzuia 10%
 
Mwacheni aongee. Mnataka kumtengenezea ili asiweze kusema ya kwake ya rohoni? Mwacheni aropoke analojisikia na sisi tupate kunufaika na huo umbea wake
 
Mi namuelewa,haya maisha ya unafiki kufichaficha yameifikisha nchi pabaya,mi sikumchagua lakin namuelewa aisee,amethubutu kuwanyooshea kidole mtu yeyote bila yoga,kongole mh mag

Hujui unaloongea au una uwezo mdogo wa kuelewa mambo, ripoti ya makinikia iliwataja akina Chenge, Yona, Karamagi nk, na akaagiza wakamatwe, je amewahi kuthubutu kutekeleza hilo? Suala la escrow ndio liliwaweka kina Regemalila ndani, je chain ya watu wa serikalini mbona hajawagusa? Anaweza kuwanyooshea vidole vidagaa na wale alio na visasi nao tu. Kinyume na hapo ni mcheza siasa za karne iliyopita.
 
Kipindi cha kutengenezewa hotuba na kikundi cha mafisadi kimeshapita, saivi ni kipindi cha kuelezana wazi tu juu ya uozo uliokuwepo, na ni muhimu uhubiriwe kila siku ili watu waelimike.
baki na ujinga wako. raisi wa nchi haropokiropoki tu. ivi unajua impacts za kiuchumi na kijamii tunazopata kwa kuhamia dodoma wewe mbwiga?
 
Wamsaidie pia aache kusema Uongo
 
Mimi ni Kada Ndakindaki wa chama na shabiki wa Magufuli wa kufa ,kasoro ulizoziahinisha ni Sawa japo ni chache,Mfano:::Ulipofika hapa kwetu lahela uliamuru walioachiwa na mahakama Kwa dhamana wakamatwe. Je watapelekwa Polisi Kwa mashitaka mapya? Au GEREZANI kutokea uraiani? Napata shida shida Sana, Mbona umeingilia uhuru wa mahakama mkuu? Tulia baba Sisi wapiga kura tunakupitisha Kwa kura Za kutosha
 
Magufuli "Mendeleo hayana chama" huyohuyo "Kamuulize diwani au mbunge wako kuhusu maji siku nyingine mjifunze"🏃🏃🏃🏃
 
Rais hana huo unafiki, unataka anyamazie uozo wa TANROAD kwakuwa tu alikuwa boss wenu?. Anayajua madudu ya TANROAD tangia akiwa huko, kwa sasa acha aisafishe.
 
Ziara zake zina tija sana...

Kuna sehemu akikukuta madudu anayafyekelea mbali hapo hapo...


Cc: mahondaw
 
Ni rais mzuri, lakini wakati mwingine ana lugha za kukera utafikri siyo kiongozi hasa kwa maeneo yale yanayoongozwa na wapinzani, anaongea umoja wa kitaifa lakini kwa maneno yake mwenyewe yeye ndiye anayesambaratisha umoja wa Taifa,na maneno yake ya kukera na kuudhi.

Na hiki ndicho kinacho wafanya wapinzani wakache mikutano yake kwa kuwa hakuna kitu cha maana zaidi ya kutolewa lugha za maudhi.

Hata misaada yake katika maeneo yanayoongozwa na wapinzani anaitoa kwa masimango utafikri waliochagua wapinzani siyo watanzania na hawana haki ya kupewa msaada na serekali yake.

Misaada yake ni ya manyanyaso hata wale wanaoomba kusaidiwa,nafuu wangekuwa wanakaa kimyaa wakabaki na heshima yao kuliko kusaidiwa kwa kudhalilishwa.
 
Umeshamaliza kutambaliza kunako unyabeni?
 
Wewe jamaa ni noma....huogopi kutekwa???!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…