Wasafiri wa mabasi nani mtetezi wetu?

Wasafiri wa mabasi nani mtetezi wetu?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,556
Kabla hujakata tiketi ya kusafiri na basi unapokelewa kwa kugombaniwa na madalali pamoja na ma ajenti waliopo katika zile ofisi zao mpaka unajiona kuwa wewe kweli ni mfalme, lakini kero zinakuja kukupata unapoanza safari na basi hilo.

Kero ya kwanza ni kwa madereva na wasimamizi wa gari hiyo kutokufikiria kuwa wamebeba binadamu ambao wana mahitaji ya mwili ya asili yaani kwenda haja, ikizingatiwa Safari nyingi huanza mapema alfajiri wakati mtu anakua hajaamka vizuri, kibaya sasa abiria kama umepanda basi mfano Stendi Kuu ya Ubungo Dar unaenda kuruhusiwa kwenda haja ndogo Morogoro.

Na kwa mwendo wa siku hizi hapo itachukua masaa hata zaidi ya matano na mkitoka hapo ni mpaka Dodoma. Hayo ni zaidi ya mateso, angalau kungewekwa angalau kila interval ya masaa matatu wasimame walau dakika 7, lakini wapi, abiria mnakua kama mmetekwa vile.

Kero nyingine ni kwenye zile sehemu ambazo mabasi husimama kwa abiria kupata vyakula au vinywaji hizi highway motels. Hawa nao pamoja na wengi kujitahidi kutoa huduma za kuridhisha za vyoo tatizo lao linakuja kwenye bei za vyakula, sijui hizi bei wanapangiwa na nani. Ni Kama bei zipo pale kumkomoa abiria kwa kuwa wanajua hatakua na muda wa kwenda pahala pengine; matokeo yake unapewa bei za ajabu.

Ati andazi 1000/=, Sambusa 1000/=, Chai ya kahawa u-mix na maziwa 2000/=, Chips yai 7,000/=. Sasa hii ni nini?

Matokeo utokaji wa vyakula hivyo unakua mdogo kitu kinachopelekea vibaki kipolo wanakuja kuchanganya na vingine vitakavyopikwa kesho na kiviuza tena. Tabia hiyo ni mbaya na hatari kwa afya za wasafiri.

Swali: Ni mamlaka ipi ya kututetea sisi wasafiri wa mabasi ya route ndefu za mikoani?
 
Mkuu mm nilishawahi fikiria hizi hotel za njian wakina nani wana masirahi humo? Maana zile bei haziendani na uharisia, hizo chips kuku wizi kabisaaa.

Ifike mahala hili jambo liwe mjadala mkubwa maana jamaa wa hizo hotel wanaibia watu.
 
Siku hizi nikisafiri nabeba juisi, sambusa au mkate na kuku, maana njiani bei ni kubwa sana mpaka unashangaa.
 
Siafiki gari kusimama hovyo.

Nadhani sheria iwekwe gari ziwe na vyoo vya haja ndogo ndani.

Labda itokee mtu ana shida nyingine kubwa zaidi basi ana haki gari kusimama kwa ajili yake.

Tena gari isimame wakati wa kula au mizani tu. Sioni haja ya gari kusimama watu wakachimbe dawa. Kwanza ni kuchafua mazingira.

Vyakula vya njiani asilimia kubwa havipo fresh. Vingi vinakuwa vinauzwa vya jana ake.
 
ibanezafrica,

Kwa upande wa chakula sikuungi mkono ebu angalia gharama za uendeshaji wa hiyo migahawa ikoje; unafikiri insendeshwa kama vile vi cafe pale Ubungo? Ukishindwa gharama chemsha mihogo viazi kahanga nyama kwako hifazi vizuri uta enjoy mwanzo mwisho.
 
ibanezafrica,

Kwa upande wa chakula sikuungi mkono ebu angalia gharama za uendeshaji wa hiyo migahawa ikoje; unafikiri insendeshwa kama vile vi cafe pale Ubungo? Ukishindwa gharama chemsha mihogo viazi kahanga nyama kwako hifazi vizuri uta enjoy mwanzo mwisho.
Zile si Five star hotels hizo gharama za uendeshaji zinatoka wapi? Mbona wangepata watu wengi tu ikiwa wangeweka bei ambazo ni reasonable?
Sasa wanagonga bei kwakua wanunuzi wengi tunawakwepa
 
Zile si Five star hotels hizo gharama za uendeshaji zinatoka wapi? Mbona wangepata watu wengi tu ikiwa wangeweka bei ambazo ni reasonable?
Sasa wanagonga bei kwakua wanunuzi wengi tunawakwepa
Hivi kama ile migawaha ya njia ya moshi arusha ukijumlisha wingi wa wafanyakazi walinzi tena kutoka ktk makampuni ya ulinzi alafu unatakiwa uuziwe msosi kama kwenu tandale huku!kama uwezi nunua mihogo ubungo fullsana autasumbuka na biashara za watu mbona sie watu ze laga popote tunapiga gambe bila kusumbuana na wahusika wa bei
 
Ttzo sio bei ni vyakula haviendani kabsa na bei na uhalisia wake kisa watu wananjaa ndo maana wanauza watakavyo yani nihovyo kabsa
Vyakula vimepoa mixer viporo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom