Wasafiri tuliowahi kupekenyuliwa/ kupigwa ndole Uwanja wa Ndege wa Mwl J.K. Nyerere Dar tuje hapa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Shida ni kwamba, huwa mizigo inapokelewa /kushushwa mapema na separate kabisa na wewe uliye ndani ya ndege na begi lako dogo.

Mara kadhaa ninapokuwa natoka Dubai, China au South Africa huwa siwi na amani na mizigo yangu kutokana na wizi wa mara kadhaa ambao vijana wa (Swisspot) pale Uwanja wa Ndege wanapopiga ndole a.k.a searching.

Unakuta ukijisahau tu ukaweka camera, saa, simu au vitu vidogo kubebeka, imekula kwako. Na sijui huwa wanajuaje kwamba begi husika lina kitu wanachotaka. Mara nyingi huwa hawakosei. Wakichana begi, lazima wakute "mtonyo". Ukilalamika unakuwa unapoteza muda tu.

Dawa yao ni kukaa na vitu vya thamani ndani halafu lile begi kubwa unaweka nguo za hovyo ikiwezekana matambara ukiwa umefunika nyoka aina ya black Mamba au mawashawasha.

Huwa washenzi sana wapiga ndole pale JNIA Dsm.

Take care.

Kama umewahi ibiwa tupe dondoo kidogo na mbinu za kuepuka.
 
pole mkuu

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app

Wale watoto uwizi hauzuiliki!!Wanalipwa mishahara midogo sana halafu wanakutana na mabegi yana vitu vya thamani lazima watuibie ili kufidia pengo la kipato chao.

Lakini si huwa kuna maelekezo kuwa vitu vya thamani kama saa,simu na laptop weka kwenye hand-luggage!!Sio Dsm tu (JNIA) wanaoiba hapo Nairobi ni balaa,O.R. Thambo ndio usiseme Dubai ndio washenzi sana
 
Kwenye baadhi ya viwanja vya ndege huwa kuna huduma ya kufunga mizigo na kamba flani kama tape hivi... Kipindi natoka china nilizungushia bag zima na lilikuwa bonge la bag... Nahisi waliona kuanza kukata zile tape watapoteza muda.

Even a black folk hate to see another nigga made it..
 
Shida ni kwamba, huwa mizigo inapokelewa /kushushwa mapema na separate kabisa na wewe uliye ndani ya ndege na begi lako dogo.

Mara kadhaa ninapokuwa natoka Dubai, China au South Africa huwa siwi na amani na mizigo yangu kutokana na wizi wa mara kadhaa ambao vijana wa (Swisspot) pale Uwanja wa Ndege wanapopiga ndole a.k.a searching.

Unakuta ukijisahau tu ukaweka camera, saa, simu au vitu vidogo kubebeka, imekula kwako. Na sijui huwa wanajuaje kwamba begi husika lina kitu wanachotaka. Mara nyingi huwa hawakosei. Wakichana begi, lazima wakute "mtonyo". Ukilalamika unakuwa unapoteza muda tu.

Dawa yao ni kukaa na vitu vya thamani ndani halafu lile begi kubwa unaweka nguo za hovyo ikiwezekana matambara ukiwa umefunika nyoka aina ya black Mamba au mawashawasha.

Huwa washenzi sana wapiga ndole pale JNIA Dsm.

Take care.

Kama umewahi ibiwa tupe dondoo kidogo na mbinu za kuepuka.

Hata pale Kia Airport sio pazuri mkuu
 
Mwaka 2014 wakati naondoka Bongo kwenda Ulaya.....jamaa waliniambia nivue saa yangu pamoja na laptop yangu niweke waiscan pale kwenye ule mkanda. Nikafanya hivyo, at the same time wengine kwa makusudi wakawa wananisemesha na kunipoteza malengo ili waniibie kumbe mwenzao nilishatonywa na jamaa yangu anayefanya kazi pale. Ile kugeuka kuangalia vitu vyangu nikaona jamaa wa Swissport kabeba simu yangu anaondoka nayo. Nikamrukia na kumtandika bonge la kichwa na kumpiga loba anipe simu, kujitetea akasema aliichukua ili akaicheki chumbani kwao. Kuja polisi na kuwaelezea kilichojiri wakaanza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe nami nikajisepia zangu huku jamaa akikanda pua yake kutokana na majeruhi. Dawa ya wafanyakazi wa swissport ni kuwaua tu au kuwakomesha kwa kichapo cha kufa mtu ndipo wataacha wizi.
 
Wale watoto uwizi hauzuiliki!!Wanalipwa mishahara midogo sana halafu wanakutana na mqbegi yana vitu vyq thamani.Lazima watuibie ili kufidia pengo la kipato chao.

Lakini si huwa kuna maelekezo kuwa vitu vya thamani kama saa,simu na laptop weka kwenye hand-luggage!!Sio Dsm tu (JNIA) wanaoiba...hapo Nairobi ni balaa,O.R. Thambo ndio usiseme....Dubai ndio washenzi sana
Mkuu hizo airports zote umetembelea?? Au umeweka maoni ya watu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wacha waendelee kujbebea Milap top, simu hata nguo mnazonunua huko ng'Ambo. Hakuna namna
 
Kuna cku tumetoka zetu nje huko na mizigo yetu sasa kuja kuichukua pale kwenye mkanda tukakuta begi zimechanwa Wameiba daa.
Kilichotusaidia mtoto wa kikwete miraji alikuwepo kwenye hiyo ndege bana nae walijichanganya wakampiga cm ya bei mbaya alikuwa amenunulia zawad baba yake Daa kilichofuata sote tulipata vitu vyote. Kuanzia cku hiyo kila nikisafir lazima juu ya begi langu naandika jina kubwa la kiongoz yoyote mkubwa nakuwa safe.
 
Back
Top Bottom