Ni kawaida ya wasafiri wa safari ndefu kusimamisha basi porini na kujisaidia maarufu kama kuchimba dawa.
Sitaki kukubali kwamba ni stahili ya msafiri kundelea kuchimba dawa katika karne hii, kwa mfano safari ya mbeya kuanzia tarehe 1 Sept 09 ni zaidi ya masaa 14 sababu ya speed limit ya 80km/phr na mizani na ukaguzi kila katika mji mdogo. Hii maana yake kila mtu atahitaji japo mara moja kuchimba dawa.
Kama kawaida, Tanzania hakuna anayehusika lakini inadhalilisha sana utu wa wasafiri, manake wake kwa waume, wakubwa na watoto vichakani tena mnaonana sababu mmebanwa hakuna anayejali.
Wanasiasa na waandishi wako busy na mafisadi lakini kuendelea kuona watu wakijisaidia vichakani si sawa, kwanza ni hatari sana kwa magonjwa ya milipuko na uharibifu wa mazingira, kwa mfano mbele kidogo ya njia panda ya mzumbe kuna sehemu wanauza nyama choma halafu ndio hapo hapo abiria wanachimba dawa na wamepewa dk 10 na konda.
Ingekuwa mafua ya nguruwe kutoka nje mpango mkakati ungetengenezwa kukabiliana na mlipuko lakini hii abiria anachukua time na kuugulia aendako. Yote tisa kumi hizo hotel ambazo zina matundu yasiyozidi manne ya choo nje kuna basi zaidi ya 10 na abiria anapewa dakika 10 kula na kujisaidia.
Binafsi ningetoa wazo kwa wajasiriamali humu jamvini, kama kuna mtu anamtaji au anaushawishi katika mifuko ya hifadhi za jamii basi asisite kuwekeza katika vyoo njiani, manake wachina katika olimpiki walitengeneza magorofa kwa ajili ya vyoo tu.
Choo na faragha ni muhimu katika maisha ya binadamu wa leo. Taasisi za kutetea haki za kinamama na mazingira ningetegemea wangekuwa mstari wa mbele kupinga utaratibu wa kuchimba dawa, mbona kuna vyoo katika ndege ili watu wajisitiri wakiwa safarini katika mfumo wa kiungwana zaidi.
Nawasilisha kwa mawazo mapya tufanyeje ili tusiendelee kuchimba dawa safarini, ni hatari kwa afya na uharibu wa mazingira ukichukulia kundi kubwa la watu kwa mara moja watu hawana maji au toilet paper za kujifutia na wanarudi vitini.
Tukumbuke barabara zetu ni za kimataifa na watu kutoka mataifa mbali mbali wanapita na kutushangaa na kushangaa hii style yetu isiyostaharabika na kukubalika.