Viongozi wote wasafi ndani ya CCM wanamfuata Jemedari mzalendo, Edward Lowassa. Njiani wapo kina Kngunge, Kinana, Karume, Nchimbi, Sitta, Tibaijuka na wengine wadogo kwa wakubwa zaidi ya 1000.
Asante Kikwete kwa kuboresha demokrasia kwa kupunguza kama sio kukisambaratisha chama kilichooza.
Ndugu yangu katika siasa chochote kinawezekana. Mimi nilitokwa povu sana kila nilipoona post inayoelezea uwezekano wa Lowassa kuhamia chadema nilikuwa napinga kwa nguvu zote kuwa hawezi. Natumia fursa hii pia kumwomba radhi mzee TupaTupa nae nilimpinga vikali sana alipoteremka na uzi wa kuwa Lowassa atahamia chadema/ukawa.Kama alivyosema m/kiti wa chadema ni kuwa hiki chama ni cha kila mmoja na kina kanuni na taratibu zake. Watakaomfuata Lowassa chadema ni wengi. Wanachama wengi,wabunge na madiwani wengi. Wengi wao watatokea ccm ambako utaratibu wao ni tofauti kabisa na chadema.Watalelewa na chadema na kufuata taratibu za chadema. Chadema ni jiko na lina wapishi mahiri na kinachotoka huko kinakubalika kwa viwango vyote.Angalia tofauti iliyopo kati ya wabunge wake na wale wa ccm. Na hata hao wa ccm tunaowaona dhaifu ni kuwa wanafanywa dhaifu kutokana na mfumo wa chama chao na huo huo ndio unaoongoza serikali yao iliyoshindwa kila nyanja.Serikali inayoogopa kuwawajibisha mafisadi na wezi wa fedha na rasilimali za taifa eti nchi itatikisika. Eti wezi walipe walichoiba na hawatashtakiwa mahakamani. Wakija chadema unaweza usiamini ni wale wale wa mipasho na wakata viuno bungeni. Sasa hivi yatasemwa mengi na wale wasiojitambua na wasiotaka kuuelewa ukweli kimakusudi tu ila ukweli unabaki pale pale kwamba Lowassa ni jembe hata kama asingehamia upinzani na kwamba sio fisadi kama wengi wanavyoaminishwa. Lowassa alijiuzulu kisiasa na wala hiyo richmond haikuwahi kuuza serikalini hata unit moja ya umeme na serikali haikuwahi kuilipa hata senti moja richmond.Ukumbuke mara ya kwanza sakata hili likianza bunge lilimwagiza mkuu wa takukuru kufanya uchunguzi wa kina kuona kama serikali ilipata hasara yoyote kutokana na mkataba wa richmond ambao ulikuwa umeshafutwa na seikali pia kuona kama waziri mkuu alinufaika na mkataba huo. Baada ya uchunguzi mkuu wa takukuru nd. Hosea alitoa taarifa kuwa serikali haikupata hasara yoyote na wala waziri mkuu hakupata faida ya kimaslahi kutokana na mkataba ule ila taratibu za uchunguzi wa kampuni ile ki-uwezo hazikuwa zimefanyika. Pamoja na taarifa hiyo bado bunge chini ya spika Sitta wakaunda kamati ya bunge ikiongozwa na Harisson Mwakyembe kulichunguza tena upya suala hilo hilo. Taarifa yao iliwahoji wengi kasoro waziri mkuu ambae hakuwa safari kwa kipindi chote na kutoa taarifa sawa na ya takukuru ila mwishoni walimalizia na kumpa Lowassa ushauri wa yeye kupima aidha kubakia na nafasi yake au kuwajibika kisiasa. Kwa yeyote ni lazima angewaza kuna wenye uchu na nafasi yake ya uwaziri mkuu.Mosi ni kuundwa kwa kamati mbili za uchunguzi juu ya suala moja. Pili wajumbe wa kamati ya Mwakyembe kutomhoji chochote anachokijua juu ya richmond hadi kuipeleka ile taarifa bungeni.Ukumbuke wote hawa walikuwa chini yake ki-utawala na walikuwa hawajapewa vyeo vya uwaziri. Mwisho kumpa ushauri wa kuchagua kati ya mawili kubaki na nafasi yake au kuwajibika kisiasa. Ni baada ya yeye kutafakari na kuona wapo wanaoutaka uwaziri mkuu wake na kuamua kujiuzulu kisiasa.Sasa naelewa wapo team Lumumba watakaotokwa povu sana na kujaribu kuniquote. Nitamjibu tu yule atakaeleta hesabu(data) za ufisadi wake na hasara aliyoisababishia nchi na hatua zilizochukuliwa kwa miaka yote minane.Tumeona kila ufisadi unaoibuliwa na data tunawekewa. Vinginevyo sitataka blablaa. Tuseme ni kweli hata majuzi hapa hamkumsikia Mwakyembe akikiri mwenyewe kuwa yale yalikuwa ni mambo ya kisiasa zaidi ila haupo ukweli unaomwonyesha Lowassa kuwa ni fisadi? Wala hamkumsikia Sitta akisema hana neno na Lowassa? Wenye kuijua sayansi ya siasa hawawezi kushabikia upuuzi .
Mkuu mleta mada umesema ukweli usio na shaka kwamba kilichotakiwa hapo ni uwaziri mkuu. Na baada El kujiuzulu tuliona waliomsimamia kooni wakipewa vyeo mbali mbali vya uwaziri na ukuu wa mikoa.