Wasabato wamuunga mkono Rais Magufuli 100%

Wasabato wamuunga mkono Rais Magufuli 100%

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,303
KANISA la Waadventista Wasabato, Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC), limesema linaunga mkono kwa asilimia 100 jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika jitihada zake za maendeleo, ikiwemo kupiga vita na kutokomeza dawa za kulevya nchini.

Askofu na Mwenyekiti wa Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC), Mchungaji Herbert Nziku, alisema kanisa hilo linaunga mkono serikali kwa vitendo ambapo linaendesha kampeni ya kupinga usafirishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya. “Tatizo la dawa za kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu wengi wameathirika na janga hili...Tusipokubali kufanya uamuzi wa busara katika kuunga mkono juhudi za serikali yetu za kupambana na biashara na matumizi ya dawa hizi, kuna hatari kwa jamii yetu na Taifa letu la Tanzania kugeuka kuwa jalala na wodi za waathirika wa dawa za kulevya,” alisema.

Alisema: “Kanisa la Waadventista Wasabato linamtaka kila mtu na kila taifa kushiriki katika kutokomeza mlipuko wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya ulioenea duniani kote, biashara ambayo inashusha hadhi ya jamii katika mataifa na kuwaangamiza walioathirika na kuwafanya waishi maisha ya uhalifu”.

Nziku alisema kanisa linatambua kuwa kufanya biashara, matumizi mabaya na kusafirisha dawa za kulevya ni chukizo mbele za Mungu, ni hatari kwa afya za watumiaji, hukosesha furaha familia na jamii, hudhoofisha nguvu kazi ya taifa na kuzidisha umasikini katika taifa.

Alitoa mwito kwa wazazi, walezi na walimu kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuikinga jamii dhidi matumizi ya dawa hizo na kuiomba serikali kupitia wizara zinazohusika kuandaa mitaala ya somo hilo kuanzia shule za misingi hadi vyuo vikuu.


Chanzo: Habari Leo
 
Kwenye hii thread wataanza kujadiliwa Wasabato wenyewe kuliko kile walichokisema.
 
Ni KWEELI...mmmmnnhhh Nadhani kwa upande wangu, Wana support jitihada za Raisi na sio kukubaliana na jambo la POLITICS+RELIGION, hilo ni against the CODE OF CONDUCT ya kanisa.
 
Viongozi wa dini walikuwaga zamani, walioko leo ni wachumia tumbo tu kama walivyo wachumia tumbo wengine wa chama cha makinikia
 
Chanzo "Habari leo" za kuambiwa changanya na za kwako
 
Kichwa cha Habari kimechanganya Mada
Hapo ilitakiwa iwe Wamuunga mkono vita ya Madawa
 
Hivi kuna watu bado wanaamini kwamba hii vita ilikua ya kweli
 
Back
Top Bottom