Warioba usitishike

Mtingaji

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
1,223
367
Kumekuwa na maoni tofauti toka kwa watu na taasisi mbali mbali ya kumpongeza na kupinga Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sintakwenda kwa undani sana lakini nitajikita zaidi kwa wale wanaotoa MAONI ya KUPINGA NA VITISHO kwa Jaji Warioba.

Kwanza wote wanao pinga wamesahau kuwa "Tume ya Warioba" ilikuwa INAKUSANYA MAONI ya wananchi nchi nzima. Imefanya kazi hiyo, ikayachuja kulingana na kipi kimependekezwa na wengi ndicho kilicho wekwa kwenye mapangilio mzuri na kuletwa kwetu tena wananchi ili tujuwe NI KIPI WENGI WAMEKIPENDEKEZA kiwemo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.

Hawa wanao mpinga na kumtisha Jaji Warioba, iwe ni individual person au taasisi yeyote ile hasa hizi za kisiasa, wana lao jambo! Huwenda wanaona maslahi yao yata vurugwa au kuzibwa ndo maana wanapiga kelele. Wananchi wote tulipewa nafasi sawa ya kutoa maoni yetu iwe kwa kuzungumza kwenye mikutano ile au kwa maandishi. Wengine Tume iliwafuata kwa heshima zao au kwa heshima ya makundi yao katika jamii ili watoe maoni yao kwa uhuru zaidi. Abaye hakutoa maoni basi ama alishindwa kwa sababu ya shughuli zake ama alipuuzia kwa sababu zake binafsi au kushawishiwa.

Kwa hiyo Tume ya Warioba ilichokitoa ndiyo MAONI YA WATANZANIA WENGI. Na ilikuwa si lazima maoni ya kila mtu yaingie kwenye Katiba kama yalivyo. Kwenye mikutano ya kutoa maoni yalitolewa maoni mengi sana mpaka ya kunyonga mafisadi, lakini hayawezi kuingia kwenye Katiba kwa jinsi hiyo. Leo mtu anapinga eti tu kwa sababu maoni yake ama ya taasisi yake hayamo jinsi walivyotaka. Hii elimu yetu ya akina Mulugo inaleta shida sasa!

Kwa sasa hivi kinachotakiwa ni kwa wananchi WACHANGIE MAONI YA KUBORESHA kile kilicho pendekezwa na WANANCHI WENGI (Rasimu). si kuleta hoja mpya, mnamtisha Jaji Warioba aliyefanya kazi nzuri na ya kupigiwa pongezi. Watu waisome na penye mapungufu watolee mapendekezo ya kupaboresha zaidi. Kama kuna jambo limesahaulika, liwekwe bayana. Kama mtu haelewi kifungu zaidi aombe msaada wa kufafanuliwa na Tume.

JAJI WARIOBA USITISHIKE
kwani kuna baadhi tumekwisha waona Rasimu imewachanganya, kwani nchi itakuwa na misingi imara ya kuongoza tofauti na sasa hivi, mambo ni urafiki na undugu. Hakuna huduma hata moja inayotolewa na serikali bure. Hakuna maadili ya uongozi ni vurugu la Wizi na ufisadi wa mali za wananchi. Mikataba mibovu mpaka wananchi wanaamua kupambana na serikali yao kwa kuona wataibiwa rasilimali katika maeneo yao.

GHARAMA ZA SERIKALI TATU ni za kawaida kama KUNA MAADILI, lakini kama hakuna maadili hata ikiwa Serikali Moja ni matatizo. Mfano sasa hivi kuna mawaziri > 60 na usafiri ni magari ya kifahari. Posho wanazo peana kwa kazi zao za kila siku ni kufuru! Pesa za miradi ya maendeleo zinavyoibwa ni aibu, forgery za nyaraka mbalimbali za mishahara hewa, miradi na tenda hewa huwezi amini-hakuna uwajibikaji-Mwizi hawezi kamata mwizi mwenzake labda wazurumiane. Safari za viongozi zisizo na tija hadi aibu. Budget za kuzikana na vitafunio maofisini usiseme, Semina, warsha, makongamano na workshops ni nyingi zisizokuwa na tija. Gharama kubwa zina kwenda kwenye mambo yasiyo kuwa na maana kabisa.

SERIKALI TATU ni jambo la muafaka kabisa, ikiwezekana kwenye Katiba ya Tanganyika tupendekeze na Serikali za Majimbo ili kusiwepo wa kumlaumu mwenzake. watakao fuja rasilimali zao kwa kuweka mikataba ya kifisadi ni wao wenyewe na si kulaumu serikali kuu.

Jaji Warioba usitishike. Watanzania tusiogope serikali Tatu. Nakumbuka baadhi ya Wabunge wa CCM kwenye mjadala wa kuanzisha vituo vya television walipinga sana eti Tanzania bado sana visianzishwe. Kumbe walikuwa hawataki watu waone wanavyolala bungeni na maendeleo duni wanayojisifia majukwaani. Na amini na hawa nao watazoea na wataona ni jambo jema kuwa na serikali tatu.
 
Back
Top Bottom