Nakumbuka kabla tume haijatoa rasimu ya kwanza, Chadema walipaza sauti zao wakiituhumu tume kuwa inaandaa rasimu yenye maslahi ya CCM, ikafika kipindi hadi wakamkashifu Jaji Warioba. Baada ya rasimu ya kwanza na ya pili kutoka wakala matapishi yao kwa kuipongeza tume. Sasa hivi wajumbe wa bunge maalumu la katiba wapo Dodoma wakiendelea na mapitio ya rasimu iliyowasilishwa na tume. Kama kawaida Chadema akiongoza kundi la Ukawa, pamoja na watu wengine wamerudia staili ileile kwamba kinachotengenezwa Dodoma ni katiba ya CCM. Nashangaa kuona hata Jaji Warioba yupo mstari wa mbele kusema ni katiba ya CCM. Tuwe wawazi na wakweli, mrejesho wa kilivchoamriwa kwenye bunge haujatolewa, tunapata wapi ujasiri wa kusema ni katiba ya CCM? Nashindwa kuelewa hata utashi wa Jaji Warioba umepotelea wapi kiasi kwamba ameamua sasa kuwa mwanasiasa. Sioni sababu ya kufanya mahitimisho wakati hata ripoti hatujapewa. Isitoshe hata kama hao CCM wataweka yao, wahusika wa mwisho na wenye maamuzi ni sisi wananchi wenyewe, kama tutaona haitufai tutaikataa, CCM si Mungu kwamba wao wanachokisema lazima sisi tukifuate.