Warioba na Rasimu Ya Watawala (Punda Afe mzigo wa bwana ufike)

Kocho

Senior Member
Jun 5, 2013
120
21
Ndugu zangu wana Jf naomba kuwasilisha hii mada kama mzalendo ktka taifa hili, kwa uoni wangu sioni mantiki ya hii rasimu hasa kipengele cha serikali ya shirikisho (serikali tatu) kwa sababu imejaa ulaji kwa watawala hasa ccm na viongozi wao kuna haja gani ya kuutetea muungano na kumbebesha mwananchi mzigo wa gharama za kuendesha serekali yenye mambo saba huu ni ujinga na zaidi ya upuuzi, hivi hawa viongozi wetu wanafikiri hizi ni zile zama zao na Mwalimu Nyerere kudumisha fikra za mwenyekiti, warioba na ccm wamesahau kuwa hayo mambo saba ndio ugomvi mkubwa katika huo muungano wenyewe kwa nni wasije na rasimu ya kutatua tatizo badala yake ndio wanaongeza matatizo mmi naona tunakoelekea ndio kubaya zaidi ya tulipotoka, hoja ni katiba ya wananchi sio katiba ya watawala ccm kwani hii nchi sio mali yao na hili ndio tatizo na kukosa maendeleo Tanzania na ndo maana wa Zanzibari wanataka kujitoa ktk huu muungano hawaoni faida za kiuchumi zaidi ya faida za kisiasa na hii ni mbaya zaidi siasa nyingi zinaligharimu taifa ktka rasilimali muda, muda mwingi watawala wetu wanatulisha siasa zaidi kuliko kutuletea maendeleo. warioba akumbuke mwisho wa siku ssi wananchi ndio tutaziendesha hizo serikali na kuwalipia hao viongozi na serikali zote kwa ujumla asilete siasa ktk maslahi yetu kama haiwezekani kuwa na muungano asitulazimishe kulipia serikali ambayo hayo mambo aliyoyaita ya muungano yanaweza kufanywa na kila upande bila kuathiri ujirani mwema na kuendesha mambo yetu kupitia EAC. wapo hapa chanel 10 eti wanasema tuna mambo saba tuuuuuuuuuu ya muungano tena wanaongea kwa kujiamini eti (punda afe mzigo wa bwana ufike) Watakufa wao mwaka huu Punda hafi wala mzigo haufiki. !!!TANGANYIKA HURU, ZANZIBAR KWANZA!!!:israel:
 
Kumbuka mkuu hii ni rasimu(draft) tu,maoni yako bado yanahitajika usiishie humu JF tu but lengo lake tume ni mzuri

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kweli kaka huu si muda wa kumtii mwenye kiti
Na km usemavyo yale mambo yenye mzozo ndio wameyarudishia pale pale kwenye serikali ya muungano
Aisee hapa wamekopi na kupesti
 
Kumbuka mkuu hii ni rasimu(draft) tu,maoni yako bado yanahitajika usiishie humu JF tu but lengo lake tume ni mzuri

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
ni sawa kaka hii ni draft ila kuna haja gani ya kuunda tume na njia nyepesi ya kutatua tatizo ipo tunaharibu pesa za walipa kodi bure ukiangalia walipa kodi wenyewe tabani tunaambiwa tunaishi chini ya dola moja, watawala wetu hawatabiriki na kutenda haki kwao ni sawa na sungura kumkaba tembo wasizunguke mbuyu wakati ukweli wanaujua tatizo ni muungano sio serikali.
 
Back
Top Bottom