ndugu wapendwa madaktari,poleni sana kwa msukosuko unaoendelea.
nawapongeza kwa kufikisha ujumbe wenu kwa watanzania na watawala.
Nina ushauri kwenu jiono hii,sikiliza.
Nakuombeni mrudi kazini,mimi nauona mgomo wenu kama ni ombi kwa baba na hakika amekusikieni hata kama hamjaonana mkaongea (mmepishana)
Tafakarini madhara/matokeo ya keshokutwa kwa familia zenu.kwa kweli itakuwa ni kiama kwenu.
Acheni kugombana na mzazi wenu,kwa kuwa mlishaonana na mawaziri nina imani madai yenu yameshamfikia waziri mkuu.
Wahudumieni watoto wenu,mama zenu,wajomba zenu na hasa dada zenu ambao ni wajawazito na sasa wameyaweka maisha yao mikononi mwenu kama ndio wakombozi pekee.
Ndugu Madaktari wote na wale wenye mapenzi mema,
Nimepata habari za kusikitisha kwamba PM amekwanda kukutana nanyi bila mawasiliano ya karibu na viongozi wenu na kukuta hamko ukumbini. Kama kawaida ya watawala wetu (ambao kiukweli walitakiwa kuwa viongozi), ametoa maagizo yake. Kwamba lazima mrudi kazini kesho Jumatatu na ambaye hatarudi kazini amejifukuziisha. Pia inasemekana amepiga marufuku mikutano yote ya madaktari.
Huu ni uthibitisho mwingine wa matumizi ya nguvu kupita kiasi kama ambavyo serikali imezoea kufanya huko nyuma. Nawaomba mpime uzito wa maagizo ya PM kwa kulinganisha na madai yenu. Natambua kuwa katika hali kama hii, ni rahisi watu kuanza kufikiria kitakachowakuta kesho au kesho kutwa baada ya kufukuzwa kazi. Ila naomba mtambue kuwa dokta habanwi kufanya kazi ya serikali. Kwa hiyo mnaweza kutumia ujuzi wenu mahali pengine lakini mkiwa watu wenye hadhi na heshima inayolingana na taaluma yenui
Ila kama mtaona kuwa bila kufanya kazi serikalini hakuna maisha tena, basi nawashauri mrudi kazini kesho asubuhi na mapema. Hata hivyo kama hilo litatokea, basi mjue kuwa huo ndio utakuwa mgomo wenu wa mwisho kabisa labda baada ya kizazi chenu kuisha.
Mungu awabariki madaktari wetu na awape uvumilivu na busara/hekima ili mpiganie hatima yenu wenyewe na generations zote za madaktari wa nchi hii.
God bless you all,
Dark City,
Ushauri mzuri sana naungana nawe kwa yote isipokuwa kuwashauri kesho asubuhi wawahi kazini, kama ulivyosema hii itakuwa mwisho wa migomo yao na dharau kubwa kwa taaluma yao, nadhani hakuna haja ya kuogopa, endeleeni na mikutano yenu wawatumie FFU. Shime madaktari msijidhalilidhe kwa vitisho vya huyu aliyepinda.
Ndugu Madaktari wote na wale wenye mapenzi mema,
Nimepata habari za kusikitisha kwamba PM amekwanda kukutana nanyi bila mawasiliano ya karibu na viongozi wenu na kukuta hamko ukumbini. Kama kawaida ya watawala wetu (ambao kiukweli walitakiwa kuwa viongozi), ametoa maagizo yake. Kwamba lazima mrudi kazini kesho Jumatatu na ambaye hatarudi kazini amejifukuziisha. Pia inasemekana amepiga marufuku mikutano yote ya madaktari.
Huu ni uthibitisho mwingine wa matumizi ya nguvu kupita kiasi kama ambavyo serikali imezoea kufanya huko nyuma. Nawaomba mpime uzito wa maagizo ya PM kwa kulinganisha na madai yenu. Natambua kuwa katika hali kama hii, ni rahisi watu kuanza kufikiria kitakachowakuta kesho au kesho kutwa baada ya kufukuzwa kazi. Ila naomba mtambue kuwa dokta habanwi kufanya kazi ya serikali. Kwa hiyo mnaweza kutumia ujuzi wenu mahali pengine lakini mkiwa watu wenye hadhi na heshima inayolingana na taaluma yenui
Ila kama mtaona kuwa bila kufanya kazi serikalini hakuna maisha tena, basi nawashauri mrudi kazini kesho asubuhi na mapema. Hata hivyo kama hilo litatokea, basi mjue kuwa huo ndio utakuwa mgomo wenu wa mwisho kabisa labda baada ya kizazi chenu kuisha.
Mungu awabariki madaktari wetu na awape uvumilivu na busara/hekima ili mpiganie hatima yenu wenyewe na generations zote za madaktari wa nchi hii.
God bless you all,
Dark City,
Nakumbuka wakati wa utawala wa Mwinyi kuna wanafunzi pale UD waliwahi kufanya madudu wakafukuzwa wote.
Upo wakati pia sikumbuki ilikuwa ni awamu ya nani pale mhimbili waliwahi kutimuliwa madaktari wote.sasa madaktari msipambane na dola.RUDINI KAZINI HUKU MKIENDELEA KUTUMIA DIPLOMASIA KUDAI HAKI ZENU.
Huu ni uchochezi sasa... hebu tuwaache madaktari waamue wenyewe jamani... wakifukuzwa utawasaidia kupata hizo nafasi???
Mkuu mie nakubaliana nawe. Sasa hivi madaktari wanahitaji kuwa na mshikamano wa hali ya juu ili kupambana na hii Serikali dhalimu. Natumai hiyo kesho wataendelea na mgomo na kutokubali vitisho vya kipumbavu toka Serikali dhalimu.
Nimewahi kushiriki katika migomo mingi tangia nipo A level hadi chuo. kuna migomo ambayo nilishiriki kikamilifu na kuna migomo ambayo nilishiriki kama sehemu ya jumuiya. Sasa huwa unafika wakati kama huu ambao linatolewa tamko kwamba kufikia kesho ingieni madarasani na kama mtu hataingia darasani basi amejifukuza. Hatua hii huwa ni kimbembe manake hapa ndipo wana mgomo hufarakana baada ya kufikiria wametoka wapi wanategemewa na nani na mipango yao ni ipi! Wengi hurudi nyuma.Usilete vitu vya kusadikika na ambavyo hauna uhakika navyo!
Nimewahi kushiriki katika migomo mingi tangia nipo A level hadi chuo. kuna migomo ambayo nilishiriki kikamilifu na kuna migomo ambayo nilishiriki kama sehemu ya jumuiya. Sasa huwa unafika wakati kama huu ambao linatolewa tamko kwamba kufikia kesho ingieni madarasani na kama mtu hataingia darasani basi amejifukuza. Hatua hii huwa ni kimbembe manake hapa ndipo wana mgomo hufarakana baada ya kufikiria wametoka wapi wanategemewa na nani na mipango yao ni ipi! Wengi hurudi nyuma.