Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,061
- 79,423
WARAKA WA KWANZA KWA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Mwana wa Nyota ya Tibeli, nalikuandikia haya nikiwa Njombe, Kwa amri ya Mungu wetu aishiye sirini, mola wetu mlezi.
Kwa Mhe, Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Neema na iwe juu yako, na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe juu yako.
Kama nilivyomuandikia Waraka mara kadhaa Hayatti John Pombe Magufuli(Mungu amrehemu) enzi za uhai wake ndivyo nitakavyotekeleza wajibu wangu kwako, kukuandikia yakupasayo kufanya uwapo katika utawala wako, wala sitakuonea wivu, wala sitokunyima haki yako ya heshima kama Mungu wangu aishivyo, wala sitakuonea HAYA wala sitakuogopa kukuandikia kwa sababu huu ndio wajibu wangu kwako. Ndio maana nalisema; kama nilivyoandika enzi za Hayatti Magufuli kwani naye sikumuonea haya wala sikuogopa, wala sikumnyima haki yake ya heshima.
Basi nipate kibali machoni pako, unisikilize kwa umakini, tena uruhusu hekima yako itende kazi, kwa maana kwako sitafuti cheo, wala sifa, wala Faida, wala mamlaka yoyote kama baadhi ya wengine wafanyavyo, pengine ningetafuta hayo nisingekutendea haki, tena ningekuonea HAYA, na KUKUOGOPA.
Haya nisikilize;
Mfalme hatawali kwa mabavu au kwa nguvu bali hutawala kwa HEKIMA na HAKI
Mfalme atawalaye kwa mabavu au kwa nguvu kamwe hawezi kutawala, na utawala wake hauwezi kudumu, tena utakuwa ni utawala wa taabu kwake. Kwa maana penye mabavu na nguvu kuna Dhuluma, uonevu, unyanyasaji, ubaguzi, umwagaji wa damu, masononeko, vilio, utumwa(ukosefu wa uhuru) na mateso ya namna zote.
Mhe, Samia suluhu jiepushe na utawala wa mabavu, utawala wa nguvu kwa maana hakuna atawalaye kwa nguvu akatawala kwa amani. Bali wewe umuombe Mungu akupe hekima ili uweze kutawala watu wake, kwa maana penye hekima ipo busara, haki, amani, utulivu, Faraja, vicheko, kujali, matumaini, na uhuru. Tena utafute watu wenye hekima, akili, busara, wacha Mungu, wenye elimu, ujuzi na maarifa hao ndio wawe watu wako wa karibu wa kukushauri ili uweze kuongoza taifa hili moyo wako ukiwa na amani.
Mtawala atawalaye kwa nguvu na mabavu hupenda kusifiwa, na hata washauri wake na watu anaowateua wamsaidie kuongoza hupenda sifa ambazo hazina maana, tena sifa hizo huwafanya wengine wawe watumwa na mateka na ambaye hasifii hujikuta katika taabu. Lakini wewe, ndiye. Mhe. Samia usiwe mtu wa kupenda kusifiwa kwa maana kwa kufanya hivyo ni kuwageuza watu mateka wako, tena kwenye sifa kuna UNAFIKI, na kwenye UNAFIKI Pana CHUKI na kwenye Chuki pana USALITI, na Penye Usaliti pana ANGUKO KUU. Basi jiepushe na kupenda kusifiwa sifa ili usijejikuta katika mtego mwishowe ukaangamia kama mpumbavu.
Bali wewe penda kujinyenyekeza, maana mtawala ajinyenyekezaye huinuliwa na Mungu na kuwa kama Jua ling'aalo kwenye barafu. Lakini mtawala apendaye kujiinua na kujitukuza huanguka na kuangamizwa, tena ipo mifano mingi ya Watawala waliopenda kujitukuza na matokeo yake waliangamia, basi jichunge sana.
Chunga sana Ulimi wako, usipende kuongea ongea sana, kwa maana kwenye wingi wa maneno ndipo upumbavu ulipojificha. Tena ulimi wako usiseme kwa unafiki, wala usiiache hekima ikapishana na ulimi wako, usije ukawabagua watu katika taifa lako.
Mhe, Samia Suluhu, kama ilivyoandikwa katika magombo ya zamani, naomba ninukuu;
Zingatia maneno niliyo yakoleza(Bold)
Zaburi 72:
1Ee Mungu, umjalie mfalme uamuzi wako,
umpe mwanamfalme uadilifu wako;
2atawale taifa lako kwa haki,
na maskini wako kwa uadilifu.
3Milima ilete fanaka kwa watu wako,
vilima vijae uadilifu.
4Mfalme awatetee wanyonge wa taifa,
awasaidie watoto wa fukara,
na kuwaangamiza watu wadhalimu.
5Mfalme aishi muda mrefu kama jua,
na kama mwezi, kwa vizazi vyote.
Mhe. Samia Suluhu kwenye utawala jambo la kwanza ni hekima, na jambo linalofuatia ni Haki na Uadilifu. Huwezi kuongoza taifa pasipo mambo hayo, ukikiuka kimoja madhara yake ni makubwa kwako na kwa unaowatawala.
Zingatia pia maneno yaliyokolezwa;
Kumbukumbu la torati 25:
13 Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. 14Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. 15Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 16Kwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu.
Mhe. Samia Suluhu, Maneno niliyokoleza yanakukumbusha kuwa, utendaji wa haki unapaswa uwe sahihi, usimpendelee mtu, wape watu wote kwa haki, na ukifanya hivyo Mungu anakuhakikishia kuwa utaishi maisha marefu katika nchi yako. Kinyume cha hivyo ni kuwa atakuangamiza ikiwa hutatenda kwa haki. Hata hivyo Mungu anasema anachukia watu wadanganyifu, ukiwa mdanganyifu kaa ukijue kabisa unamchukiza Mungu.
Udanganyifu wa Watawala ukoje?
Watawala waovu hupenda kujikosha wawapo mbele ya makutano, mbele ya majukwaa, mbele ya Vyombo vya habari na Kamera; wakijifanya ni watu wema na watu huwashangilia kwa sababu ya unafiki wao wa kujivika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Yesu anawaambia watu wa namna hii ni kama makaburi ambayo kwa nje yamepakwa chokaa na marumaru lakini ndani yake ni mifupa ya wafu na uchafu wa kila namna.
Mhe. Samia Suluhu, jiepushe na tabia za makaburi yaliyopakwa chokaa, tunafahamu utakuwa na wapambe na wapakaa chokaa, ambao watakupamba na kuremba kwa kila kitu hata kama ni kibaya wakakiremba kionekane kizuri. Watu wanaweza kukupenda kwa kuwa tunajua kuwa watu wengi hupeperushwa na upepo wa kile kisemwacho kwenye Media.
Tabia za wapaka makaburi chokaa na wasafisha vikombe kwa nje, huwazuia wengine wasiuseme ukweli, huunda sheria za kukandamiza uhuru wa kujieleza ili ukweli usifahamike. Mhe. Samia Suluhu, jiepushe na hao Wapaka chokaa Makaburi kwa nje.
Kwenye Utawala jambo la kwanza ni haki. Haki ndio huzaa uhuru, uhuru ndio huleta maendeleo. Hakuna taifa lenye maendeleo bila ya haki. Maendeleo hujikita katika furaha za wananchi, huwezi kuvunja haki kwa kisingizo cha maendeleo. Ila unaweza vunja maendeleo kwa kisingizio cha haki. Majengo, barabara, hospitali, elimu, na maendeleo mengine yasiguse haki za watu. Utakapomaliza utawala wako, Mungu hatakuuliza ulileta maendeleo bali atakuuliza ulitenda haki.
Kwa Mungu Haki ndio maendeleo, kwa shetani maendeleo ndio haki.
Neno haki ni pana sana. Haki ndio maendeleo.
Mhe. Rais, kamwe usijekubali ukamwaga damu ya mtu yeyote hasa asiye na hatia. Ndio maana unapaswa uwe makini katika kuteua wapambe na wasaidizi wako, kwa maana usipokuwa makini unaweza ukashangaa wapambe na wasaidizi wako wakakuangusha, na hakika lawama zote zitakuwa juu yako, kwa maana itahesabika wewe ndiye ulimwaga damu kwani wewe ndiye uliyewateua, ndio maana nalikuambia uchague watu wacha Mungu, wenye hekima, elimu, ujuzi na maarifa. Usichague watu wapenda sifa na madaraka.
Mhe. Samia Suluhu, kuna kanuni inasema usishindane na tu mwovu, naomba pia hii uizingatie katika utawala wako. Usijikite katika kupambana na adui zako usijejikuta umeingia mtegoni. Watawala wote waliojikita katika kuhangaika na mahasimu wao waliishia kuangamia wao wenyewe. Ndio maana Yesu alisema; Usishindane na mtu muovu. Bali iache sheria itende kazi sawa sawa na inavyosema. Hata hivyo nafahamu kuwa waovu huwa na akili mno, ikiwa ni hivyo basi ili upambane nao nawe yakupasa utumie akili, kamwe usitumie nguvu kubwa. Tumia akili ukimuomba Mungu.
Mhe. Samia Suluhu, mimi Taikon nitaendelea kukusapoti kwa mema utakayo yafanya, walakini utakapokengeuka na kutotenda haki, naiahidi nafsi yangu, na kukuahidi na wewe kuwa nitakuandama kwa makaripio, makemeo na maonyo kwa kadiri ya nafasi nitakayopewa na Mola wangu. Wala sitaogopa kukuonya ikiwa utatenda isivyo haki. Nami nitakutumaini ikiwa utatenda sawa sawa na Haki, kwa kufuata sheria na maagizo ya Mungu, na kwa utashi wa mwanadamu ukifuata sheria za nchi. Lakini sitakutumaini wala hutakuwa kitu mbele ya macho ya Mungu na mbele ya macho yangu ikiwa hautatenda kwa haki.
Mwisho wa Yote, Nakuombea kwa Mungu akupe hekima ya kutawala watu wake kwa haki.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Njombe

Mathayo 23:27
“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo yanapendeza kwa nje, lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu.Watawala waovu hupenda kujikosha wawapo mbele ya makutano, mbele ya majukwaa, mbele ya Vyombo vya habari na Kamera; wakijifanya ni watu wema na watu huwashangilia kwa sababu ya unafiki wao wa kujivika ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Yesu anawaambia watu wa namna hii ni kama makaburi ambayo kwa nje yamepakwa chokaa na marumaru lakini ndani yake ni mifupa ya wafu na uchafu wa kila namna.