Mechi ya Tanzania kukamilisha ratiba iko saa ngap wadau?
Angekuwa mzalendo zaidi kwa kukataa uteuzi na kutoa hizo sababu zake.
ni kweli mkuu hawa wachezaji wanafki sana
Kwanza hana weredi,huu waraka alitakiwa autoe baada ya kumaliza idadi ya mechi walizotakiwa kucheza
Mmeusoma ujumbe wa Boko, nafikiri ndio. Sasa je unafiki wake ni Unafiki upi? kutokukataa mwaliko?. Kwa nini tunajiaminisha kwamba kugoma ndio njia pekee ya kuwasilisha ujumbe?? Vipi kama angefungiwa na TFF kwa kukataa kuipigania nchi?
Kila mtu anamapungufu, ila mwenye busara hujaribu kuyatafuta, kuyajua na kuyafanyia kazi mapungufu yake.
Boko na wenzake wamejaribu ila wameona hii haiwezekani. Njio tunayotumia sio, tunazidiwa maarifa na ujanja sehemu. Maelezo yake si jambo jipya, wengi wameshashauri hayohayo. Je ulitaka Boko ndio aanzishe shule za soka??
......,hujiulzi kwanini wanaitana kindugu na wachezaji wazuri wanaachwa?lazima kuna figisu wanazozificha hawa wachezaji maandazi
Unamzungumzia Boko au wenye mamlaka ya kuteua team ya taifa? Sikubaliani na Kocha na uteuzi wa ovyo anaofanya ila ni nani ambaye ana kiwango tofauti sana na wenzake ambae ameachwa???
Tatizo kama nchi hatuzalishi wachezaji wazuri, tulionao uwezo upo limited na hilo ndio Boko analosema (Akiwemo bojo mwenyewe).
Anachoshauri ndio wadau wanaofatilia soka yetu wanakuwa wanashauri kila siku. Kwangu ni faraja kubwa kuona this time ni mchezaji ( from the horse mouth) ndio anazungumza. Inanipa faraja ukizingatia na uelewa wa wachezaji wetu.