Waraka wa elimu kuhusu VITABU vya kiada

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
765
Tukisoma waraka unaoitwa: “Waraka wa elimu na. 4 wa mwaka 2014 kuhusu utayarishaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia” – ambao mtu anaweza kuupata kwenye tovuti ya Taasisi ya Elimu (Tanzania Institute of Education), utaratibu wa uandaaji wa vitabu vya Kiada (textbooks) kwa ajili ya elimu ya nchi yetu umewekwa wazi.

Umepangwa katika hatua kuu 3:

1. Uandishi wenyewe (writing of books)

2. Uhakiki wa Maudhui (Validation of contents)

3. Utoaji wa ithibati (Approval)

Na unaeleza kuwa mhusika kwenye kila hatua ni nani.

Mimi naamini kuwa hatua zote zilifuatwa kwa kuwa sidhani kama wataalamu wetu hawa wanaweza kufanya jambo kubwa kama hili (elimu ya nchi yetu) bila kufuata utaratibu unaohusika.

Lakini kwa kuwa pamoja na kufuata utaratibu huu, walichotuletea ndicho hiki ambacho kila mtu amekiona au kukisikia sasa (yaani vitabu vilivyojaa makosa mengi), je, haujafika wakati ambapo elimu ya nchi iache kuchezewa na nchi iache kupotezewa wakati?

Utangulizi wa “Waraka” unasema wazi:

“Kabla ya mwaka 1991, jukumu la kuandika vitabu lilikuwa la Serikali kupitia Taasisi ya Elimu (TET) ambapo kitabu kimoja cha kiada kilitumika kwa kila somo kwa shule zote za Tanzania Bara.”

Baada ya utaratibu huo kushindwa kufanya kazi, uliachwa. Leo tunataka kurudi kulekule! Je, ni sawa? Hivi akitokea mtu leo akasema, “Tunarudisha viwanda vyote, mabenki yote, makapuni ya simu yote – mikononi mwa serikali” itakuwa ni sawa?

Naamini jukumu sahihi la serikali kwa jumla na Taasisi ya Elimu lingebakia kusimamia viwango. Ruhusu watu waandae vitabu lakini komaa kwenye viwango. Kitabu kinachofaa kipite; kisichofaa kitupwe kapuni.

upload_2017-5-16_9-10-46.png
 
Back
Top Bottom