Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 610
Nimekutana na Waraka unaohusu Uraia Ndumilakuwili, nikashindwa kuvumilia kuusoma peke yangu.
"...Kwa hakika katika zama hizi Tanzania inakumbwa na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi ambayo nilidhani Mheshimiwa Jakaya aliingia kwenye madaraka ili atuongoze kuyatatua. Naamini kuwa akiwa kama msomi wa historia anajua fika kuwa hawa watoka mbali wanaopendwa sana na viongozi wetu wa sasa wameitumbukiza nchi kwenye lindi la umasikini uliokithiri; vijana wetu wanazagaa mitaani bila kazi wala ajira kwa kuwa uwezo wa nchi wa viwanda ulisambaratishwa na serikali ya awamu ya tatu; madawa ya kulevywa yameingizwa kwa wingi nchini; ukimwi na maradhi mengine ya kisasa yameshamiri; aidha kwa kutumia dhana ya utandawazi vijana wetu wamegeuzwa kuwa malimbukeni wa mila mbovu za magharibi zinazopembejewa na vyombo vyote vya habari mchana kutwa na usiku! Nilidhani uongozi makini ungekerwa na hali iliyopo na kufanya kila jambo kuleta mabadiliko ya kudumu yenye tija kwa nchi. Kinyume na matarajio inaelekea kuwa viongozi wetu sasa wanaedeshwa na ajenda za wakubwa wa dunia ambao ajenda yao si kumjenga na kumboreshea maisha Mwafrika bali kumnyanganya uhuru wake na rasilmali zake ili arudi katika hali ya utumwa na ukoloni; hali ambayo mataifa makubwa (ambayo sasa yana matatizo makubwa ya kiuchumi) yanapenda kuziweka nchi zote za Afrika kwa ajili ya kupora rasilmali zake!..."
Imekaa vizuri hii habari- soma attachment!