Waraka mfupi sana kwa Wantanzania

Waraka mfupi sana kwa Wantanzania

mbozimbozi kumwitu

Senior Member
Joined
Mar 8, 2025
Posts
158
Reaction score
187
Ndugu zangu na watanzania wenzangu ni matumaini yangu mbukheri wa afya na km haupo sawa Mungu akupe nguvu,Amina.

Kwa Leo nimewiwa kuongea na watanzania wenzangu wapenda maendeleo na wazalendo wa kweli wa nchi hii Tanzania.

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu,pamoja na uchaguzi mkuu Tanzania tumekuwa na matukio ya hovyo sana ya watu kutekwa,kupigwa na kuumizwa na kuuwawa na kupoteza kwa watu.

Kama Mtanzania nimekuwa naumizwa sana na matukio ya kupoteza kwa watu kisa TU mtu anatoa maoni yake ambayo yapo against TU na serikali, jaman tumefka mbali sana na sijui tunatengeneza kizazi Cha namba gani,wanaouwawa wana family pamoja na Watoto sijui Watoto zao watajiskia kivip?? wakiambiwa kuwa baba yako aliuwawa kisa alikuwa anaikosoa serikali.

Tukitaka nchi yetu tuwe na maendeleo,lazima tuwe na democracy ya kweli ndio itatuletea maendeleo lakini sio kuwa na chama kimoja chenye nguvu kuliko vingne.leo hii tukingekuwa na vyama viwili vyenye nguvu sawa hii nchi ingekuwa mbali sana,

Chadema sio mda wa kutengana, ni mda wa kuwa wamoja sana na kuwa na uthubutu,slogan yenu ya no reform no election ni nzuri sana pambaneni sana inaweza kutujengea Tanzania mpya,tupo nyuma yenu japo not easy..

G -55 nawaita wasaliti kwenye vita...

Mungu tulinde na Mungu tupiganie..
 
Back
Top Bottom