Supporter wa viboko hapa. viboko ni vizuri ila sasa nyinyi walimu chapeni idadi inayoeleweka ya viboko
shida yenu kwanza haumshikiri mtoto kwenye kosa lake-maana wewe unaweza kuwa umeona dogo ana kosa lakini dogo kumbe ana fact zake zinazoweza kuwa za kweli au sio za kweli. wewe humpi nafasi ya kusikiliza na kupima hoja zake.
s'tyms dogo anaweza kuwa na hoja za kweli wewe haumpi nafasi ajielezee unang'ang'ania kumchapa tu. sasa yule ni binadam na hakuna kitu kinauma kama kuadhibiwa kwa kitu ambacho hujafanya. hilo ni moja.
mbili, walimu wengi mnachapa idadi isiyoeleweka ya viboko. yani ni kama unaua nyoka vile na unatanguliza hasira mbele. hii sio sawa na ndo maana mnaishia kuambiwa mna stress. wewe chapa viboko vinavyohesabika na ikiwezekana umwambie kabisa dogo "kwa kosa hili utachapwa viboko kadhaa". viboko ni njia nzuri tu kumrudi mtoto hasa kwa jamii zetu za weusi ila nyinyi walimu ndo mmeviharibu mnatumia vibaya.