mrxtz2026
New Member
- Jan 24, 2026
- 3
- 1
Imetolewa:
Dodoma, Tanzania
29 Januari 2026
Kumb. Na: Maoni/JMT/01
Ndugu Mheshimiwa,
Napenda kuchukua fursa hii kuwasilisha barua hii kwa heshima na uzito unaostahili, ikiwa ni sauti ya mwananchi na mchango wa kitaaluma unaolenga mustakabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Napenda kukujulisha kuwa maoni haya ya Katiba nilihusika kuyawasilisha katika misingi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ikulu Mawasiliano, Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na semina na majukwaa mbalimbali ya kiraia na kiserikali yanayohusiana na masuala ya Katiba, sheria, na maendeleo ya Taifa.
Nimeamua kuchukua nafasi hii kueleza kwa uwazi kuwa, kwa kuzingatia hali inayoendelea nchini, mahitaji ya marekebisho ya Katiba, misingi ya utawala wa kisheria, pamoja na malalamiko na matukio yaliyoibua hisia za hofu, sintofahamu na kutojiamini kwa wananchi katika mifumo ya uchaguzi, kuna haja ya kuchukua mchakato huu wa Katiba mpya kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mpana, na maridhiano ya kweli.
Ni muhimu mchakato wa Katiba kuzingatia masuala ya msingi yanayohusu: mgawanyo wa madaraka, uwajibikaji wa viongozi, uhuru wa mihimili ya dola, haki za msingi za binadamu, mifumo ya uchaguzi iliyo huru na haki, pamoja na uimarishaji wa utawala bora kwa maslahi ya Taifa.
Kwa kuzingatia historia ya nchi yetu na uzoefu wa awamu mbalimbali za uongozi, naamini Katiba itakayopendekezwa inapaswa kuakisi matamanio ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo, badala ya kulinda maslahi ya kundi au watu wachache.
Natoa wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa maoni ya wananchi yanakusanywa, yanachambuliwa kwa haki, na yanazingatiwa kwa dhati katika rasimu ya mwisho ya Katiba. Vilevile, elimu ya uraia iimarishwe ili wananchi waelewe vyema haki na wajibu wao katika mchakato huu muhimu wa kitaifa.
Nina imani kuwa uongozi wako utaona umuhimu wa maoni haya kama mchango chanya wa kizalendo unaolenga kujenga Taifa lenye haki, amani na maendeleo endelevu.
Naomba kuwasilisha.
Wako katika Kujenga Taifa,
Dodoma, Tanzania
29 Januari 2026
Kumb. Na: Maoni/JMT/01
Ndugu Mheshimiwa,
YAH: MAONI YA WANANCHI KUHUSU PENDEKEZO LA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

“Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mungu awabariki wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”