Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,159
Inanibidi niandike waraka huu kwako binafsi kutokana na uonevu unaoendelea nchini, wakati wewe ndiye Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Mhimili ambao sisi wanyonge tunautegemea kwa kutenda haki
Ninaongelea kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) na mwenzake Masonga.
Watuhumiwa hao wawili wametoa maombi yao kwa Hakimu anayesikiliza kesi yao Hakimu Mteite ya kumwomba asiendelee kuisikiliza kesi hiyo.
Wametoa sababu 3 ambazo wanaamini zingezingatiwa basi Hakimu huyo asingeweza tena kuendelea na kesi hiyo.
Sababu zenyewe ni kama zifuatazo:-
1.Ingawa tuhuma yao inadhaminika kisheria, lakini Hakimu huyo ameamua kupindisha sheria na kusema wao waendelee kusota ndani. kwa madai kuwa eti usalama wa Watuhumiwa hao utakuwa shakani!
Je yeye Hakimu amejuaje kuwa kuna watu wanaopanga kumdhuru Sugu kama siye yeye na wenzake??
2.Ni haki ya Watuhumiwa kuiambia Mahakama kuwa hawana Imani na Hakimu iwapo wataona dalili za kuwa Hakimu huyo haelekei kuwatendea haki
watuhumiwa na maombi hayo kikawaida huwa yanazingatiwa
.
Lakini cha ajabu katika kesi hii ya akina Sugu, Hakimu ameng'ang'ania kuwa ataisikiliza hadi mwisho!
3.Watuhumiwa walimsikia wenyewe Hakimu huyo akitamka kuwa kesi hii "inampa wakati mgumu" ambayo ni ushahidi tosha kuwa kuna shinikizo toka upande wa wanasiasa kutaka hukumu iwe ya aina fulani wanayoitaka wao.
Tunakumbuka kuwa Jaji Mkuu ulitoa onyo Kali kwa wanasiasa kuwa kuanzia sasa Mahakama yako mtakuwa wakali sana kwa yeyote anayetaka kuingilia Mahakama katika utendaji wake wa kazi za kila siku.
Naamini utayazingatia niliyoyaongea katika waraka huu.
Ni Mimi mwananchi wa kawaida