Wapinzani wanaomfagili Kikwete kwanini hawarudi CCM!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapinzani wanaomfagili Kikwete kwanini hawarudi CCM!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 24, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  ....badala ya kujifanya ni Wapinzani kumbe ni Mamluki!? Cheyo na Mrema wakati umefika sasa wa kurudi CCM na kuacha usanii wenu wa kujifanya nanyi pia ni Wapinzani.

  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  MATOKEO ya ripoti ya Shirika la Utafiti la Synovate yaliyotolewa juzi yamewagusa watu wa kada mbalimbali wakiwamo wa vyama vya upinzani,baadhi wamekiri kumkubali Rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wengine wanadai ni uongo.

  Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amekiri kwamba, CCM na viongozi wake wanakubalika kwa kuwa wameota mizizi kwa muda mrefu.

  Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameponda matokeo hayo akisema ni uongo na ufisadi mtupu.

  Lipumba amelinganisha utafiti huo na utabiri wa Mnajimu maarufu, Shehe Yahya Hussein wa Dar es Salaam.

  Amesema, matokeo ni ya kupanga na mtu anayefahamu masuala ya takwimu, atabaini kwamba ni uongo uliotungwa kwa ajili ya kumfagilia Rais Kikwete.

  Ametoa mfano kwamba,katika uchaguzi mdogo uliopita, waliopiga kura walikuwa si zaidi ya asilimia 30 kwa maana kwamba ni vigumu utafiti huo wa Synovate kuonesha kuwa asilimia 94 ya wananchi walisema wako tayari kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

  Cheyo amesema,matokeo hayo yaliyoifanya CCM kupewa asilimia nyingi yanaifanya ijiimarishe zaidi kwa ajili ya uchaguzi ujao.

  “Sipendi kusema moja kwa moja kuwa matokeo yaliyotolewa juu ya Rais Kikwete hayaendani na hali halisi iliyopo, wala sipendi kumzungumzia Kikwete kutokana na matokeo hayo, kwa kuwa nitakuwa nampigia kampeni, ila ukweli ni kuwa Kikwete anakubalika na wanachi wake na hata chama hicho,” amesema.

  Pamoja na kwamba hakutaka kueleza kwamba hakuna anayeweza kufua dafu kwa Rais Kikwete kwenye uchaguzi wa mwaka huu, Cheyo alisema, “mimi kwenye urais wala hata sitarajii kugombea, nitaendelea kugombea nafasi yangu hii niliyonayo ya ubunge, kwanza kuna mipango mizuri kwa wananchi wangu inayonipasa kuitekeleza,” amesema Cheyo.

  Mwanachama wa CHADEMA na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Profesa Mwesiga Baregu, alisema kukubalika kwa CCM na Rais Kikwete kunategemeana na utafiti wenyewe kuwa umefanywa katika maeneo yapi.

  Alisema unaweza kwa upande wa maeneo ya vijijini CCM au Rais Kikwete wakakubalika sana tofauti na ilivyo mijini.

  “Hata leo hii ukiuliza jambo lolote kuhusu utendaji wa Rais Kikwete, yapo baadhi ya mambo utakayoambiwa kuwa ameshindwa kutekeleza ipasavyo,” alisema.

  Akizungumzia demokrasia nchini, Profesa Baregu alisema chama tawala kimeshindwa kutoa nafasi kwa vyama vya upinzani kutawala.

  Kuhusu kukubalika kwa Zitto Kabwe, viongozi hao walisema hali hiyo imetokana na namna Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema) alivyopambana kutetea mambo mbalimbali kwa maslahi ya Taifa hili huku upande mwingine akithubutu hata kutofautiana na wanachama na viongozi wenzake wa Chadema.

  Mwanaharakati wa masuala ya amani na Katibu Mkuu wa Amani Forum, Risasi Mwaulanga alisema CCM chini ya Mwenyekiti wake Kikwete, bado ina nafasi kubwa ya kutawala hasa kutokana na jinsi ilivyo karibu na wananchi ikilinganishwa na vyama vingine.

  Alisema pia Chadema imejizolea umaarufu zaidi kwa kuwa baadhi ya viongozi wanakubalika wanapokuwa majukwaani .

  “Leo nitakwambia kuwa CCM inakubalika zaidi majukwaani kutokana na mgongo wa Rais Kikwete na uzoefu wa ujumla wa chama hicho, Chadema wao inatokana na viongozi wake kama Wilbrod Slaa, Zitto na Freeman Mbowe, lakini si kwa chama chenyewe,” alisema Mwaulanga.

  Synovate,iliyokuwa Steadman Group zamani,juzi ilitoa matokeo ya kura zilizopigwa na wananchi huku zikionesha kuwa Rais Kikwete anawaacha mbali wapinzani wake katika uchaguzi wa mwaka huu.

  Viongozi waliopitwa na Kikwete ni pamoja na Mbowe na Profesa Lipumba huku Zitto aking’ara katika ubunge.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  badala ya kujifanya ni Wapinzani kumbe ni Mamluki!? Cheyo na Mrema wakati umefika sasa wa kurudi CCM na kuacha usanii wenu wa kujifanya nanyi pia ni Wapinzani..............

  Afadhali hao wanajionyesha wako wengi mno... list can go on and on, mtu unamsifia JK! unataka nini? ndio wanaishia kutukanwa bure
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,421
  Likes Received: 2,081
  Trophy Points: 280
  Heshima yako Babu, hawa jamaa wengi wao ni vibaraka. Katika strategic management wanasema kama ukiona unapata upinzani sana ktk biashara yako, fungua biashara nyingine kama tatu ili uonekane umepata wapinzani wengine kwa majina tofauti. Watakimbia na kwenda kwingine wakidhani wanakukimbia kumbe wananunua kwako bila kujua. So babu hawa wapinzani ni walewale tu wana kadi za chama cha mapinduzi na wamelipa ada ya mwaka mara ya mwisho jana.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Vyama vya upinzani kwa maoni yangu havikuundwa ili kugombea nafasi za Ubunge tu bali pia Urais. Kama vyama vinavyojiita vya upinzani vinashindwa kusimamisha wagombea katika nafasi ya Urais basi havina haja ya kuendelea kuwepo na kuonyesha kama vile kuna upinzani kumbe ni usanii tu.

  Ni heri turudi kwenye utawala wa chama kimoja kuliko kuwa na vyama vya upinzani ambavyo ni mamluki na kila inapofikia karibu na uchaguzi wanakuwa mstari wa mbele kumfagilia mgombea wa CCM badala ya kunadi wagombea wao.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Nimesikia kuna uwezekano JK akasimama mwenyewe mwaka huu! inauma sana

  kumsifia JK ni kutaka ubunge, kua siri kubwa sana hapa, wenyeviti wa vyama hivi wakiingia bungeni , halafu wakaondoka na kiinua mgongo cha milioni 46 mchezo achilia mbali mshahara wa kila mwezi na posho za bungeni?

  kama tunavyopiga vita akia RA, EL n.k wito jamani wa kujua vyama gani ni wasaliti.maana navyo ni vya kifisadi tu

  sijasema kuhusu ruzuku ambayo ni kodi zetu, na hasa sisi wafanya kazi kodi kubwa inauma kweli!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu hivi vyama vya upinzani vinavyopewa ruzuku kwa kujidai ni vyama vya upinzani wakati havisimamishi wagombea Urais katika uchaguzi Mkuu inabidi vifutwe ili tuwe na vyama vya upinzani wa kweli au kurudi kwenye chama kimoja.

  Wanachofanya Mrema na Cheyo ni utapeli wa kujifanya ni vyama vya upinzani halafu kuvaa magwanda ya CCM karibu na uchaguzi Mkuu ili kumpigia debe Kikwete.
   
 7. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Nchi hii ina Chama kimoja tu makini cha siasa, CCM.

  Huyo Zito Kabwe wa Chadema juzi juzi tu kapewa shavu na JK leo hii tarrrrratibbb.

  Subirini muone nani atakubali kugombea urais vyama vya upinzani safari hii. Dr. Slaa, Lipumba, Mbowe, Mrema, Cheyo, Mbatia woote wanataka ubunge ili mambo yakae sawa. Narudia tena hawa niliowataja kuwathibitishia kuwa ni mamluki, hakuna hata mmoja wao atakayegombea urais mwaka huu. Naomba mliandike hili kwenye Diary zenu.

  Upinzani Tanzania ni NGO za kutafuta ruzuku na kukwepa kodi.

  CCM ndiyo chama chenye historia ya kuwajali wananchi. Kikwete ndiye Rais wetu 2010-2015. Na hata 2015 CCM itashinda na mgombea kutoka CCM upande wa Zanzibar ndiye atakaye kuwa Rais wa Tanzania.
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,464
  Likes Received: 26,353
  Trophy Points: 280
  Ninja tumekusikia na kuelewa UONO wako.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...