Wapinzani waingiza kanuni zao rasmi bungeni

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa mara ya kwanza wametoa kanuni zao ambazo zitatumika kama mwongozo kwa wabunge wanaotokana na vyama hivyo.

Kanuni hizo ambazo zimeridhiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai inaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kwa wapinzani kuwa na kanuni zao.

Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema, alisema mchakato wa kupata kanuni hizo ulipitia hatua mbalimbali ikiwemo kuwashirikisha wabunge wa kambi ya upinzani ambao walizisoma na kusaini.

Kitabu cha Kanuni hizo chenye kurasa 24, kilitolewa jana na kusainiwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na kugawiwa kwa kila mbunge wa upinzani hasa wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Tumeamua kuwa na kanuni za kuelimisha Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na awali tulifanya utafiti kwa nchi zote za Afrika hakuna kambi ya upinzani yenye kanuni ila kwa Tanzania ni ya kwanza.

“Ni matumaini yetu nchi hizo zitakuja Tanzania kujifunza namna tulivyotunga kanuni hizi, ambapo zimepitia hatua mbalimbali ikiwemo kushirikisha vyama husika na unajua Kambi inaundwa na wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa.

“Imesomwa na kila mbunge na wote wameridhia na kuisaini kila mmoja na baadae Spika wa Bunge, Job Ndugai, aliridhia kuanza matumizi yake, ninawapongeza wabunge wote wa upinzani kwa kuzikubali kanuni hizi ambazo ndizo zitakuwa mwongozo wao,” alisema Mrema

Mkurugenzi huyo wa Masuala ya Bunge wa Chadema, alisema anaamini wabunge wote wa upinzani watazifuata kanuni hizo na kuwaongoza katika majukumu yao ya kazi za kibunge.

Chanzo:
Mtanzania
 
Ni ishara wamekiri kasi ya Magufuli iawafanya waendelee kuwa wapinzani milele. Hongera zao kwa kujitambua. Lakini ninahofu Miustaadh ya CUF itakuwa imesaini bila kujua dhamira ya Mbowe ni kuwabana zaidi wao...
 
kanuni hizo zitatumika kwa muda wa miaka mingapi? wakifanikiwa kuongoza nchi kanuni hizo zitawafaa wale watakaokuwa wapinzani ambao kwa sasa hawajabahatika kupewa nakala hizo? au ndo kukubali kuwa UKAWA wamekubali kuwa wapinzani miaka yote ili mataifa mengine yaje kujifunza kuwa wapinzani wa kudumu katika nchi?
 
Ungetoa muhtasari wa hizo kanuni ingekuwa vizuri. Umetuacha tu speculate.
1. Jee zimebana uhuru wa wabunge wa upinzani, badala ya kuwakilisha wananchi wa majimbo yao (ambao wengine si wa chama chao) sasa watakuwa wawakilishi wa chama chao tu?
 
kanuni hizo zitatumika kwa muda wa miaka mingapi? wakifanikiwa kuongoza nchi kanuni hizo zitawafaa wale watakaokuwa wapinzani ambao kwa sasa hawajabahatika kupewa nakala hizo? au ndo kukubali kuwa UKAWA wamekubali kuwa wapinzani miaka yote ili mataifa mengine yaje kujifunza kuwa wapinzani wa kudumu katika nchi?
Miaka mitano ni mingi na ndio umri wa bunge hivyo kujiwekea kanuni katika kipindi hiki cha miaka mitano ni jambo la kupongezwa.
Ni kama timu ya Moira yaweza amua maimu huu wa ligi tutatumia 4-4-2 basi.
 
Back
Top Bottom