Wapinzani wachezea kichapo kibondo

Wapinzani wachezea kichapo kibondo

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
799
Reaction score
603
WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIBONDO

Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.

Diwani wa CCM Ndugu Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.

Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.

Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.

Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.

Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape.
 
Wanaccm acheni siasa nyepesi kwa upande wa madiwan upinzani sio ngome yote idadi ya ccm ni kubwa mpaka nape mwenye akili ndogo aje awasaidie ama kweli ccm kwishineyi
 
ona aibu basi mkuu madiwani wa CCM walikuwa wangapi na upinzani wangapi?14 kwa 3 alafu ulitaka ushindi?kwanza wapinzani hawakusimamisha mtu katika nafasi yoyote,acha kupotosha na kupotoka ,je mwenyekiti wenu bwana Gwegenyeza amejiuzulu ama la?uchaguzi wa leo ilikuwa sawa na baba amchunguli mama bafuni
 
Tatizo la waapinzani wa Bongo wanadhani porojo za kwenye mitandao na magazeti ndio kila kitu.

Matokeo yake ndio kama hayo. Juzijuzi walitangaza kwamba wataongoza halmashauri Kibondo na CCM itakuwa upinzani, matokeo yake yameonekana.

Hakutakuwa na tofauti 2015 baada ya uchaguzi mkuu, wataambulia kunawa tu...
 
mwambie Mbatia 2015 hakuna ubunge wa kuteuana...
 
WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIBONDO

Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.

Diwani wa CCM Ndugu Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.

Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.

Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.

Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.

Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape.
Hiyo ni cha mtoto kichapo kapokea Mwigulu - Ugaidi wa Lwakatare kashindwa, Ugaidi wa Tindikali Kashindwa na uchaguzi wa Madiwani Arusha kapigwa 4 - 0 .
 
Ungesema ni kwa hisani ya Michuzi,maana naona umehamisha hadi heading lakini huja accredit,yani huja acknowledge source ya habari.Ndo mwanzo wa plagliarism huu.
 
Tatizo la waapinzani wa Bongo wanadhani porojo za kwenye mitandao na magazeti ndio kila kitu.

Matokeo yake ndio kama hayo. Juzijuzi walitangaza kwamba wataongoza halmashauri Kibondo na CCM itakuwa upinzani, matokeo yake yameonekana.

Hakutakuwa na tofauti 2015 baada ya uchaguzi mkuu, wataambulia kunawa tu...

Kiongozi;Is this statement from you?
Kibondo CCM ina madiwani 14 na wapinzani madiwani 3 tu!CCM kushangilia kushinda kuunda serikali ya Kibondo ni jambo la kushangaza sana!

Mkuu why mnashangilia hata sehemu mliyo shinda madiwani kwa kishindo?
 
Ulisoma gazeti la UDAKU Tanzania Daima?
 
Afadhali ya Nape kuliko 'Savimbi gaidi'.Angeenda 'Savimbi', huo ushindi usingepatikana,maana hana busara ya kuwasikiliza wananchi.'Gaidi' anadhani yeye tu anajua,misifa tupu akijidai mchumi daraja I.
 
Huyu aliyeandika thread hii ana upungufu wa akili. Nini cha ajabu ukimwona mwanamke ana ujauzito? Wawezaje kushangilia hivyo hali unajua nilazima? Huu ni ulevi wa viongozi wa ccm,badilikeni akina nape mtatia aibu mshindwe kumalizia vibanda vyenu mwaka 2015
 
Uzuri wa CHADEMA ni kwamba wao tayari wamegundua kuwa hawana chao kwenye siasa na kwa sasa wanawekeza kwenye miradi mikubwa mikubwa kama kujenga mahoteli, kumbi za starehe na kuanzisha NGO nchini, ni mkakati mzuri kwa kweli.

Ushahidi;

Hotel - Pretoria hotel ya Mbowe.

Kumbi za starehe - Bilicanas iliboreshwa na kuongeza waburudikaji kwa fedha za CHADEMA.

NGO - IGEHETA ya Dr Slaa na mchumba wake Josephine, mtaji wa NGO hii ulitoka CHADEMA kwa zaidi ya 80%.
 
Tatizo la waapinzani wa Bongo wanadhani porojo za kwenye mitandao na magazeti ndio kila kitu.

Matokeo yake ndio kama hayo. Juzijuzi walitangaza kwamba wataongoza halmashauri Kibondo na CCM itakuwa upinzani, matokeo yake yameonekana.

Hakutakuwa na tofauti 2015 baada ya uchaguzi mkuu, wataambulia kunawa tu...

...kwa mitizamo kama hii naamini watu wengi watazimia na wengine kufa kabisa kwa kile kitakacho wapata 2015 toka kwa upinzani...
 
Uchambuzi mzuri unaendana na takwimu,je unaweza kutueleza CCM ilikua na viti vingapi vya Udiwani na Upinzani walikua na viti vingapi? Vinginevyo huu ni upuu.zi wa kina Nepi na wenzio kujisifia
 
Tatizo la waapinzani wa Bongo wanadhani porojo za kwenye mitandao na magazeti ndio kila kitu.

Matokeo yake ndio kama hayo. Juzijuzi walitangaza kwamba wataongoza halmashauri Kibondo na CCM itakuwa upinzani, matokeo yake yameonekana.

Hakutakuwa na tofauti 2015 baada ya uchaguzi mkuu, wataambulia kunawa tu...

Mzee ume kuwa formatted kichwani hukumbuki Arusha mwezi uliopita kilichowapata Magamba? ??
 
Back
Top Bottom