Wapinzani tutoke na kick ipi kupambana na Rais Magufuli maana kila tunalojaribu tunashindwa

Kada wa CHADEMA

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
289
615
Wapinzani tumejiloga wenyewe. Tulianza vema na sasa tunapoteza mwelekeo. Tulishindwa kujipanga vema wakati wa transition na revolution ndani ya CCM tukajikuta sisi tunakumbatia kile ambacho CCM wamekikataa. Tangu Oktoba 2015 baada ya matokeo ya uchaguzi Mkuu kutoka, tumejaribu kick nyingi sana ili angalau tuonekane tupo. Miongoni mwa kick hizo ni;

Kupinga kitendo cha Rais Kutosafiri nje ya nchi kama alivyofanya Kikwete. Kick hii ilibuma hata kabla hatujaitumia sana kwa vile hapa tulionesha ukilaza wa hali ya juu sana. Kikwete tulimpinga sana kwa kusafiri sana nje ya nchi mpaka tukampachika jina la Mr FastJet. Leo hii Magufuli amesikia kilio chetu tunamsakama. Kupinga fukuza fukuza ya watumishi.

Wakati Rais Magufuli akitimua watumishi na viongozi wazembe, wabadhilifu, majizi na mafisadi, sisi UKAWA tuliona hiyo ni kick itakayotuuza. Tukaamua kusimama kidete kuwapigania wanaotumbuliwa hata hivyo wananchi wametudharau. Hapa kick imebuma. Baada ya Bunge la Bajeti kuanza, Nape Nnauye ambaye tunamuita kilaza hakika katuzidi ujanja. Katuwekea kamtego ka kijinga sana sijui imekuwaje tumenasa kirahisi zaidi.

Nape katangaza bunge lisioneshwe live. Mishipa ikatutoka bungeni ili kupinga uamuzi huo wa serikali mpaka tukajikuta tunavunja kanuni za bunge. Sasa vyombo vyetu kama Zitto, Bulaya, Lissu nk vimepigwa ban ya muda mrefu. Bungeni sasa tumepwaya na sasa wabunge wa CCM wanajinafasi

Mkataba wa Lugumi tulidhani kuwa ni kick itakayowasambaratisha CCM. Tukatumia nafasi hiyo kutaka kutengeneza mazingira kuwa Rais anajaza rafiki zake kwenye serikali yake tukitoa mfano wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa kuna mgongano wa maslahi na hivyo Rais anashindwa kumchukulia hatua kwa kuwa ni Rafiki yake.

Magufuli kaonesha jeuri yake pale alipomfukuza Kitwanga kwa kosa la kuingia bungeni akiwa amelewa. Baada ya hapo suala la Lugumi limedoda. Ukosefu wa Sukari nchini awali tulidhani kuwa ni kick baab kuubwaaaa. Tukatumia matatizo hayo kupaza sauti tukadhani kuwa wananchi watatusikia na watatuunga mkono.

Tulidhani kuwa wananchi wataandamana. Wapiiiii. Wananchi wametulia tuliiii kwa vile wanajua kuwa Rais wao ana dhamira njema pale alipopiga marufuku uingizaji holela wa sukari nchini. Wananchi wanajua kuwa haya ni matatizo ya muda mfupi tu.

Mkwamo wa kisiasa Zanzibar. Wananchi tulitumia mkwamo huo kujijenga kisiasa. Tukafanya maamuzi ya kijinga na ukilaza pale tulipowashauri CUF wasusie uchaguzi wa Machi 20 tukadhani kuwa hiyo ni kick itakayotuuza kimataifa. Wapiiiiii. Kwa sasa CUF imekuwa kama kundi la waasi vile maana sasa wanatumia mbinu chafu kutaka kujionesha kwenye public. Tumefikia hatua ya kuhamasisha wapinzani wetu wawachukie wana CCM.

Kuanza harakati za Kumpinga Naibu Spika. Hakika huu ni ujinga na ujuha wa hali ya juu sana. Awali tulidhani kuwa Naibu Spika atashtuka. Lakini wapiii. Mbaya zaidi yamefanyika maamuzi kuwa Naibu Spika ataongoza vikao vyote vya asubuhi. Matokeo yake kila tukichungulia Bunge tunamkuta Tulia katulia tuliiii. Haooooo tunarudi kwenye vyumba vyetu na kwenye baa tukijilia vyetu huku tukiwahadaa wananchi kuwa tumesusa. Tehetehetehetehe. Wananchi sasa wametuchoka na wametudharau.

Kuwatetea wanafunzi. Serikali ilipowafukuza wanafunzi 7000 wa UDOM, sisi tukaona kuwa hiyo ni kick itakayotuuza. Tukapaza sauti kuwa hao wanafunzi wameonewa na wamenyanyaswa. Rais akapigilia msumari wa mwisho alipoongea na wananchi alipoweka jiwe la msingi ujenzi wa maktaba kubwa pale UDSM.

Sasa tumetulia tuliiii tusijue nini cha kufanya. Kuanza kushambulia familia ya Rais. Tumeanza na Jesca Magufuli na sasa tumeingia kwa Prof Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF tukidhani kuwa hiyo kick itatulipa. Dah kweli Magufuli katushika kisawaasawa

Ndugu zangu, naamini kuwa nanyi mnajua kick nyingi zaidi ya hizi ambazo tumezitengeneza ili kupambana na Rais Magufuli. Hata hivyo, nadiriki kusema kuwa tumeshindwa. Magufuli katuzidi nguvu na ujanja. Hakuna kick imetusaidia hata moja.

Ndo maana nimeamua kuweka uzi huu ili tujaribu kubadilishana mawazo juu ya ni Kick ipi itatusaidia kupambana na rais Magufuli ambaye anazidi kupanda chat kila uchwao
 
Wewe siyo mpinzani Na siyo kada Wa chadema endelea Na kazi yako watanzania wana macho Na masikio kwa hiyo wanaona na kusikia kachukue buku Saba yako muwadahili wanafunzi wenyewe muwape mikopo wenyewe serikali ya ccm Leo mje muwaite vilaza kwa hiyo wote 7802 ni vilaza akuna wenye ufaulu Wa kutosha hii zambi Mungu ndio anajua adhabu Yake kwenu
 
Hahaaa poleni sana bana...sisi huku ccm rahaa tuu tunazidi kujenga nchi na nyinyi jengeni maneno
 
Wewe siyo mpinzani Na siyo kada Wa chadema endelea Na kazi yako watanzania wana macho Na masikio kwa hiyo wanaona na kusikia kachukue buku Saba yako muwadahili wanafunzi wenyewe muwape mikopo wenyewe serikali ya ccm Leo mje muwaite vilaza kwa hiyo wote 7802 ni vilaza akuna wenye ufaulu Wa kutosha hii zambi Mungu ndio anajua adhabu Yake kwenu
Sasa ndo umeandika nini? Kama huna cha kuchangia kwenye uzi huu bora ukakaa kimya
 
Kwa mtu makini hajivui nguo hadharani, pia tumia uwezo wako kutafuta habari kamili juu ya chama kabla hujajianika hadharani, chama si kick, ni mipango madhubuti inayowekwa na kutekelezwa, bahati mbaya huwa haianikwi kama mtama.
 
Wewe siyo mpinzani Na siyo kada Wa chadema endelea Na kazi yako watanzania wana macho Na masikio kwa hiyo wanaona na kusikia kachukue buku Saba yako muwadahili wanafunzi wenyewe muwape mikopo wenyewe serikali ya ccm Leo mje muwaite vilaza kwa hiyo wote 7802 ni vilaza akuna wenye ufaulu Wa kutosha hii zambi Mungu ndio anajua adhabu Yake kwenu
Huyu ni Kada wa Chadema anayejaribu kujitambua ila tayari wameshachelewa, walibugi tangu pale walipomuuzia LOWASSA chama.
 
Sasa ndo umeandika nini? Kama huna cha kuchangia kwenye uzi huu bora ukakaa kimya
Mimi nimechanga za kuambiwa na zangu nikaona yafuatayo..
1. Umejipa jina la upinza ili ionekane wapinzani wanajisema
2. Kila uzi unaoanzisha unawasema wapinzani wakati ID yako inaonyesha wewe ni mpinzani... MALMLUKI
3. Ukiona upinzani umekushinda (KAMA KWELI NI MPINZANI) rudi CCM kama Mwapachu
4. Ni dahmbi kusema uwongo kuwa wewe ni mpinzani wakati siyo...

Nimechanganya na zangu ninaona wewe huna tofauti na Lizaboni, Rutashoborwa etc...
 
Sasa ndo umeandika nini? Kama huna cha kuchangia kwenye uzi huu bora ukakaa kimya
Ujui nimeandika nini wakati umeweza ku quote nilichoandika najue umenielewa utawala Bora auji kwa kusifiwa tu Na kukosolewa pia kunajenga serikali Bora
 
Huyu ni Kada wa Chadema anayejaribu kujitambua ila tayari wameshachelewa, walibugi tangu pale walipomuuzia LOWASSA chama.
Ni kweli kabisa Mkuu. CHADEMA na upinzani wote waliteleza toka mwanzo. Haya yanayotokea sasa ni matokeo ya mtelezo huo
 
Wapinzani tumejiloga wenyewe. Tulianza vema na sasa tunapoteza mwelekeo. Tulishindwa kujipanga vema wakati wa transition na revolution ndani ya CCM tukajikuta sisi tunakumbatia kile ambacho CCM wamekikataa. Chama kuhodhiwa na mafisadi na vilaza.

Tangu Oktoba 2015 baada ya matokeo ya uchaguzi Mkuu kutoka, tumejaribu Kick nyingi sana ili angalau tuonekane tupo. Miongoni mwa kick hizo ni;

  1. Kupinga kitendo cha Rais Kutosafiri nje ya nchi kama alivyofanya Kikwete. Kick hii ilibuma hata kabla hatujaitumia sana kwa vile hapa tulionesha UKILAZA wa hali ya juu sana. Kikwete tulimpinga sana kwa kusafiri sana nje ya nchi mpaka tukampachika jina la Mr FastJet. Leo hii Magufuli amesikia kilio chetu tunamsakama. Kweli sisi ni vilaza.
  2. Kupinga fukuza fukuza ya watumishi. Wakati Rais Magufuli akitimua watumishi na viongozi wazembe, wabadhilifu, majizi na mafisadi, sisi UKAWA tuliona hiyo ni kick itakayotuuza. Tukaamua kusimama kidete kuwapigania wanaotumbuliwa hata hivyo wananchi wametudharau. Hapa kick imebuma.
  3. Baada ya Bunge la Bajeti kuanza, Nape Nnauye ambaye tunamuita kilaza hakika katuzidi ujanja. Katuwekea kamtego ka kijinga sana sijui imekuwaje tumenasa kirahisi zaidi. Hapa sisi ndo tunaonekana vilaza. Nape katangaza bunge lisioneshwe live. Mishipa ikatutoka bungeni ili kupinga uamuzi huo wa serikali mpaka tukajikuta tunavunja kanuni za bunge. Sasa vyombo vyetu kama Zitto, Bulaya, Lissu nk vimepigwa ban ya muda mrefu. Bungeni sasa tumepwaya na sasa wabunge wa CCM wanajinafasi
  4. Mkataba wa Lugumi tulidhani kuwa ni kick itakayowasambaratisha CCM. Tukatumia nafasi hiyo kutaka kutengeneza mazingira kuwa Rais anajaza rafiki zake kwenye serikali yake tukitoa mfano wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa kuna mgongano wa maslahi na hivyo Rais anashindwa kumchukulia hatua kwa kuwa ni Rafiki yake. Magufuli kaonesha jeuri yake pale alipomfukuza Kitwanga kwa kosa la kuingia bungeni akiwa amelewa. Baada ya hapo suala la Lugumi limedoda. Kweli sisi ni VILAZA.
  5. Ukosefu wa Sukari nchini awali tulidhani kuwa ni kick baab kuubwaaaa. Tukatumia matatizo hayo kupaza sauti tukadhani kuwa wananchi watatusikia na watatuunga mkono. Tulidhani kuwa wananchi wataandamana. Wapiiiii. Wananchi wametulia tuliiii kwa vile wanajua kuwa Rais wao ana dhamira njema pale alipopiga marufuku uingizaji holela wa sukari nchini. Wananchi wanajua kuwa haya ni matatizo ya muda mfupi tu.
  6. Mkwamo wa kisiasa Zanzibar. Wananchi tulitumia mkwamo huo kujijenga kisiasa. Tukafanya maamuzi ya kijinga na ukilaza pale tulipowashauri CUF wasusie uchaguzi wa Machi 20 tukadhani kuwa hiyo ni kick itakayotuuza kimataifa. Wapiiiiii. Kwa sasa CUF imekuwa kama kundi la waasi vile maana sasa wanatumia mbinu chafu kutaka kujionesha kwenye public. Tumefikia hatua ya kuhamasisha wapinzani wetu wawachukie wana CCM.
  7. Kuanza harakati za Kumpinga Naibu Spika. Hakika huu ni ujinga na ujuha wa hali ya juu sana. Awali tulidhani kuwa Naibu Spika atashtuka. Lakini wapiii. Mbaya zaidi yamefanyika maamuzi kuwa Naibu Spika ataongoza vikao vyote vya asubuhi. Matokeo yake kila tukichungulia Bunge tunamkuta Tulia katulia tuliiii. Haooooo tunarudi kwenye vyumba vyetu na kwenye baa tukijilia vyetu huku tukiwahadaa wananchi kuwa tumesusa. Tehetehetehetehe. Wananchi sasa wametuchoka na wametudharau.
  8. Kuwatetea wanafunzi vilaza. Serikali ilipowafukuza wanafunzi 7000 wa UDOM, sisi tukaona kuwa hiyo ni kick itakayotuuza. Tukapaza sauti kuwa hao wanafunzi wameonewa na wamenyanyaswa. Rais akapigilia msumari wa mwisho alipoongea na wananchi alipoweka jiwe la msingi ujenzi wa maktaba kubwa pale UDSM. Sasa tumetulia tuliiii tusijue nini cha kufanya.
  9. Kuanza kushambulia familia ya Rais. Tumeanza na Jesca Magufuli na sasa tumeingia kwa Prof Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF tukidhani kuwa hiyo kick itatulipa. Dah kweli Magufuli katushika kisawaasawa
Ndugu zangu, naamini kuwa nanyi mnajua kick nyingi zaidi ya hizi ambazo tumezitengeneza ili kupambana na Rais Magufuli. Hata hivyo, nadiriki kusema kuwa tumeshindwa. Magufuli katuzidi nguvu na ujanja. Hakuna kick imetusaidia hata moja. Ndo maana nimeamua kuweka uzi huu ili tujaribu kubadilishana mawazo juu ya ni KICK IPI ITATUSAIDIA KUPAMBANA NA MAGUFULI ambaye anazidi kupanda chat kila uchwao
bora bangi ipigwe marufuku Tanzania. unaona madhara ya bangi hayo
 
Hahahahahaahaa Kilaza wa Division Fooo ya Thelathini hahahaaha kweli aiseeeee, hivi sukari ipo?
Wewe vilaza huwajuie, angalia hizi shahada za mwendokasi za akina Msigwa na Lema.
Mlifikiri fagio lake litawafagia CCM peke yao? Na bado mtalia sana.
 
Back
Top Bottom