Wapinzani tumieni busara kwa manufaa ya wapiga kura

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
WIKI iliyopita wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, waliweka msimamo wa kutohudhuria kikao chochote cha Bunge, kitakachoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, kwa madai kuwa anatumia ubabe na kuwapendelea wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wabunge hao wa kambi ya upinzani walisema hawataona tabu kuendelea na utaratibu huo wa kususa vikao vinavyoendeshwa na Dk Tulia hata kama itakuwa ni vipindi vyote hadi Bunge livunjwe kwa sababu lengo lao ni kupinga uonevu na ubabe anaowafanyia.

Hatua hiyo imetokana na Naibu Spika kutokubali kujadiliwa kwa hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), jambo ambalo lilikuwa tayari limetolewa ufafanuzi ndani ya bunge hilo.

Jambo la kujiuliza je, ni hoja ya kwanza kukataliwa bungeni kwa sababu mbalimbali? Kwa nini hili limewafanya kuchukua hatua kali sana kwani tayari wamepeleka kusudio bungeni la kupeleka bungeni hoja ya kumuondoa madarakani naibu spika huyo huku wakiwa wanatoka nje ya Bunge mara aingiapo Naibu Spika Tulia.

Inawezekana ya kuwa wana hoja za msingi kuhusu madai yao, lakini naona ni vema kusubiri maamuzi ya ofisi ya Bunge ambayo tayari Bunge limeeleza kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye anakusudia kuliwasilisha suala hilo kwenye kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kama kanuni inavyoelekeza na kamati ndiyo itaangalia msingi wa hoja na endapo itaridhia itawasilishwa bungeni ili kujadiliwa kwa mujibu wa kanuni.

Wakati suala hilo likiendelea kujadiliwa, wabunge wa kambi hiyo ya upinzani wameamua kutohudhuria vikao vyote vya Bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika ambaye kwa sasa anaendesha vikao vingi jambo ambalo linasababisha wabunge hao kutotimiza matakwa ya wapiga kura ambao waliwachagua ili wawakilishe katika Bunge.

Nawiwa kusema labda kambi ya upinzani wana agenda yao nyingine kwa sababu wanasusa suala ambalo linaendelea kufanyiwa kazi. Wanafanya hivyo wakati wanajua fika kuwa kitendo hicho cha kususa vikao kinawaathiri zaidi wapiga kura ambao wanakosa uwakilishi bungeni kuliko Naibu Spika.

Wapinzani wanaosusa vikao vya Bunge wanawaumiza wananchi ikizingatiwa kuwa leo ni siku ya kusoma bajeti kuu inayotarajiwa kusomwa na Waziri wa Fedha, Phillip Mpango, ikiwa ni bajeti ya kwanza katika uongozi wa serikali ya awamu ya tano. Katika bajeti hiyo wananchi wanategemea kusikia mchango wa kambi ya upinzani.

Ni vema kwa kupitia kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kutumia busara katika hilo kwa kurejea bungeni kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo hili la bajeti kuu pamoja na mengineyo ambayo kwa kutokuwepo ni vigumu kuchangia kwa maslahi ya wananchi wa majimbo yao.

Nasema busara itumike kwani tayari malalamiko yao yamesikilizwa na uongozi wa Bunge na yanafanyiwa kazi, hivyo kususa vikao ni sawa na wao kutoa hukumu. Ni vema kuendelea na kazi waliyotumwa mpaka hapo maamuzi yatakapotolewa.

Mimi nadhani kama wangechukua maamuzi ya kutoka bungeni baada ya Bunge kutoa maamuzi ingekuwa suala lingine, lakini kwa sasa naona haikuwa wakati wake hivyo kujijadili upya katika maamuzi hayo.
 
Haya ni matokeo ya upinzani uliowekeza mtajiwake wote kwenye "matukio"....ikifika kipindi matukio yameisha, wanaanza kuyatengeneza wenyewe kilazima..
 
Angalizo kwa mletamada: Mwenyekiti's word is final and unquestionable! Jiandae kurushiwa mishale ya "usaliti"...kila la kheri
 
Mleta uzi na mchangiaji..uzi mnausaka... ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa kwa nguvu zote...njaa ni mbaya sana.
 
Wambieni CCM nao watumie busara kuheshimu demokrasia kwanini wanaogopa kukosolewa wanataka kusifiwa tu?
 
Hili jambo ukiliangalia kwa makini ni kuwa serikali na Bunge ndio ambao hawana uzalendo na wanapenda Wapinzani wasihudhurie bunge.
Wapinzani wameshitaki kuhusu NS na wamesema hawatahudhuria akiwepo. Sasa kwa nini wana ng'ang'ania aingie yeye wakati kuna wenyeviti wengine watatu ukiacha spika anayeumwa?
Hapana, msiwalaumu wapinzani kwa msimamo wao bali hao wanaolazimisha Naibu aje bungeni wakati ana mgogoro na wabunge?
Sisi ndio tupige kelele akae pembeni hadi jambo hili liishe
 
Back
Top Bottom