Wapinzani sasa twalana wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapinzani sasa twalana wenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsayaMwita, Dec 4, 2009.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hakika , hakika, CCM ni vicheko na ndelemo, kile walichotegemea sasa chatimia, walijua kuwa upinzania nguvu yao ni ndogo ni kelele za chura.

  Ni kweli wapinzani walifanikiwa kuwashika pabaya ila kwa sasa kila kukicha wanajinasua pole pole,

  Hebu sisi watanzania ni nani katuloga? tumekuwa kama gari linalosukumwa mara liwake mara lizime? Daaa!!!!! sijui hatima ya upinzani.

  Kinachonisikisha ni hili jambo la ukabira linalotajwa kila kukicha, sijui uchaga, lakini ni kweli hawa ndugu zetu wachaga hatuoni mchango wao katika ujenzi wa Demokrasia hapa nchini?

  Nadhani kuna kila sababu za kuvumiliana ndugu zangu, si vema kuuboa upinzani,

  Ile hoja ya kwamba CHADEMA ndiyo chama mbadala inaanza kutoweka kila kukicha.

  Je nini hatima ya haya yanayoendelea?

  Je huu ndiyo mwisho na kusambaratika kwa chama(CHADEMA) hiki Makini?
   
 2. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mungu inusuru Tanzania na mikono ya hawa mafisadi.
   
 3. C

  Charuka Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  chura na umakini wapi na wapi.
  umakini uliharibika pale walioanza kuwaita wenzao majina ya ajabu, mara chama fulani mfu , ooh fulani sisimizi. Mkuki kwa nguruwe, 'msibate ushungu yakhe'
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  acha wasambalatike..............ndio maana muda wote mimi binafsi nimekuwa siamini ktk vyama vya siasa vilivyopo kwa kuwa kila chama kina kasoro yake ambayo ni kubwa na ambayo bila kuikubali kuwa ni kasoro na kuirekebisha basi mustakabali wake ndio kama tunavyoona yanayotokea chadema,.....................muda wote naota chama kipya kitakachoundwa na wapambanaji wa ufisadi kwani kitakuwa chama cha kitaifa zaidi kuliko hizi longolongo zilizopo..................kwa haraka haraka wamekatisha tamaa wananchi..............kama wanagombana saaizi baada tu ya kuona wanaanza kukubalika sasa ingekuwaje kama wangetwaa madaraka..............yale yaliyotokea kenya tungeyaona haraka sana....................................wa wapi wazalendo wa nchi hiiii....................nashangaaa kumbe hata vijana chipukizi waliopo bado wapo kwa maslahi binafsi inasikitisha sana............................imagine nguvu iliyokuwepo chadema afu inakuja kuishia hapa tunapoendelea kushuhudia.....mnaamini katika upinzani wa kweli?
  ccm waendelea kukenua maana vita ya panzi........furaha ya kunguru.
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  mengi aliisha sema hawa watu ni hatari sana kwani wanamtandao hadi nchi za nje na wanaweza kukuua popote utakapokuwa................kwao pesa ni kila kitu
  kweli wamefanikiwa..................wamemnunua zitto nae kawafuata akina hatu
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwa Danda na David ndiyo kielelezo cha Chadema kufa ama kuna jambo zaidi ya hili ambalo silijui ? Kama David na Danja wanakose wanasimamishwa kazi na hawaja fukuzwa uanachama utasemaje CCM wanaweza ?Kwani kuwa mwana Chadema wa kweli ni kazima uwe na madaraka ? Mie nadhani ni wakati wa kujipanga na kuendelea mbele . Chadema hawajawafukuza uanachama ila wamewavua madaraka tu kwa mambo ya kuwajibika so tatizo ni wapi ?
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  kama unafikiri chadena wanasaidika......sasa tuwasaidieje????????????????????????????mi soma alama za nyakati
   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jile

  Kwani chadema wamekuomba uwasaidie? Na hao unaowategemea wakufanyie kazi ya upinzani (wakati wewe umelala?) ni kina nani?
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Eti huyu naye ni mpinzani?!
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Isaya ulichofanya hapa hakina tofauti na akina Kafulila, Dandu au sijui nani wanaoikosoa Chadema baada ya kutoka.

  1. Chadema bado credibility yake iko juu sana kulinganisha na vyama vingine vyote ikiwamo CCM.WANACHOPITIA SASA ni kwenye tanuru, Muda huu kwa Chadema ni mzuri kuliko kipindi kingine chochote, maana wanakomaa kwa kujua hali halisi ya watanzania wakiwamo wewe

  2. Siku zote huwa nawapasha Chadema warekebishe makosa yoyote kama yapo zikiwemo nyimbo hizo za zamani sana ulizozisema hapo juu. Kuwapo kwa tuhuma hakumaanishi kusambaratika ndugu! kuna wanaume wamefumaniwa na wake zao live, tukijua ndoa itasamabaratika ndiyo kwanza inakomaa!!

  3. Post kama zako athari zake ni kuwa wengi watavidharau vyama hivi, consequently, wengi hawapigi kura! wakiamini CCM watashinda.So if you real need true revolution kosoa wazi panapoonekana na ushahidi elez wazi hisia zako ila ziwe za mjengo

  Chadema wana nafasi kubwa ya kurekebishika kama kuna tatizo ila HAITASAMBARATIKA.

  NIKIWAPA USHAURI HUWA WANAKASIRIKA

  MBOWE, ZITTO, MTEI WAKAE PEMBENI KABISA WAKIMSAIDIA MWENYEKTI MPYA , ILA ASIWE SLAA!!!
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Tatizo la baadhi ya yetu, mambo madogo wanayaona makubwa na makubwa wanayaona madogo. Hatuwezi kufika popote kwa mawazo na mitazamo hii.
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ndio mwisho kabisa...! Karibuni tena CCM
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sina uhakika kama wale wote waliopo upinzani ni upinzani kweli. Walio wengi ni wanaCCM wazuri tu, na wapo huko kwa kazi maalumu. Nawambieni ukweli kwamba upinzani wa kweli ndo upo njiani unakuja. CCM itakaposambaratika na kuisha ndipo tutapata upinzani. Hatuwezi kuwa na upinzani tukiwapo na CCM yenye mshikamano wa kweli. Maana hao CCM wana vyombo vyote vya usalama na kwa ujumla ndio wanaovilinda hivyo vyama vya upinzani ili viendelee kuwepo. Najua wengi mtanipinga, lakini CCM inajua ni nani aliye wake huko CHADEMA na si ajabu wanaopanga nani awe nani huko CHADEMA. Naamini kama Zitto pia angekuwa mteule wa CCM basi kwenye nafasi ya Uenyekiti angepita bila shida. Lakini kwakuwa "anaweza kuwa na upinzani wa kweli" dhidi ya CCM basi hakufaa kuwa mwenyekiti huko.
  Namshukuru yule aliyetuwekea humu ile orodha ya members wa kamati kuu ya CHADEMA, manake katika hao yupo mmoja ambaye ni CCM mwenzetu lakini na yeye ni member wa kamati kuu CHADEMA. Tunapoteza muda tu na upinzani wa Tanzania. Ndo maana nchi inaenda hovyo lakini hakuna anayehofu. Maana wanajua hakuna wa kuwatoa madarakani hao CCM. Maana CHADEMA wenye japo nguvu kidogo ni ndugu zao wa karibu kabisa na dili zote wanapanga pamoja. Hawana lolote hawa. Wanaiongezea umasikini tu nchi yetu.
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Si kweli kwamba hoja ya CHADEMA kama cha mbadala inaanza kutoweka hizo ni hisia zako tu.Na pia CHADEMA haiwezi kusambaratika kama unavyodhani na kujidanganya au na kutaka kutisha watu kwa makusudi. CHADEMA ni chama mbadala na kinaendelea kupanda kila inapoitwa leo......kalaghabao.
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha!Unajidanganya ndugu yangu....Uko kama mtoto mdogo anayeamini kwamba baba yake niye mtu mwenye nguvu kuliko watu wote duniani na anaamini kwamba baba yake anaweza hata kumpiga tembo bila silaha. Hebu jitahidim kuacha ushabiki kidogo na kuwa realistic,unataka kufanana na nduguyo Makamba.
   
 16. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jile79

  Ndugu hapa ndipo tutaweza kujua ni kweli siasa za Tanzania ni nini hatima yake?

  Je ndiyo ile demokrasi ya kweli imeanza kuchipua?

  Ama ndiyo tunazikwa?

  Mungu inusuru Tanzania na hawa ...........
   
Loading...