Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Vyama vya siasa vya upinzani Afrika vyenye idikadi na malengo yanayofanana viunganishe nguvu zao kwanza ili kuviondoa vyama vilivyokuwa vya ukombozi vilivyogeuka kuwa mkoloni,
Vifanye hivyo kabla yakusaka misaada toka Ulaya. Makoloni na mabeberu haya ya ndani ambayo zamani vilikuwa vyama vya ukombozi viliungana vikashinda enzi hizo... Na leo vinaungana ili kuua vyama vya upinzani. Ipo mifano mingi ya matunda ya mashirikiano, kulikuwa na mashirikiano makubwa kati ya TANU na CPP cha Gold Coast (Ghana).
Julisu Nyerere na Dr Kwame Nkrumah walifahamiana Uingereza kati ya miaka 1945, Nyerere akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Edinburgh Scotland na Nkurumah akiwa chuo kikuu cha School of Economics mjini London. Na wote kwapamoja walikutanishwa katika shirika la kijasusi la Malkia Elizabert lililo chini ya Kanisa la Anglikana liitwalo Fabian Society ambalo lilikuwa na jukumu la kuwaandaa vijana wa kiafrika kuja kuzitawala nchi zao. Katika shirika hili vijana wa kiafrika wengi walikutana hapo wakiwemo akina Netto, Mugabe, nk
Tukirudi nyuma, Mwaka 1949 Nrumah alitoka katika chama cha UGCC akaunda Convention People’s Party (CPP) iliyokuwa na madai makali zaidi. Mwaka 1951 CPP ilipata kura nyingi katika uchaguzi baada ya kudai uhuru mara moja. Nkrumah aliyekuwa tena mbaroni aliruhusiwa kugombea, alipata asilimia 98,5 za kura mjini Accra akaachwa huru. Mwaka 1952 alichaguliwa na Halmashauri ya Kisheria kuwa waziri mkuu wa koloni.
Aliendelea kuongoza serikali na mwaka 1957 wakati wa uhuru alibadilisha jina la nchi kuwa Ghana. Hii ilikuwa koloni la kwanza kupata uhuru katika Afrika ya Magharibi, baada ya Liberia. Mwaka huohuo alifunga ndoa na Fathia Helen Ritzk, Mkristo wa Kikopti kutoka nchi ya Misri.
Ni katika kipindi cha 1927 ambapo AA ilipokuwa ikiundwa na chini Rais wake Mwalimu Cesil Matola (Myao), Katibu wake Klest Sykes (Mzuru mhamiaji toka Afrika Kusini) na Mhazini wake Ali Ramadhani (Mzaramo) wa Pwani la Azania, ndipo Mwalimu Matola alipomuomba makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Accra nchini Gold Coast (Ghana) Dr Kwegyir Aggrey asaidie kuwaandikia katiba ya chama chao. Alifanya hivyo na hadi leo anakumbukwa kwa mtaa mmoja kule Kariakoo kupewe jina lake la Aggrey.
Mashirikiano hayakuishia hapo, Mwaka 1954 wakati Julius Nyerere na makomred wenzake akina Abdul Sykes, John Lupia nk wakiunda TANU, waliomba katiba ya chama cha Kwame Nkurumah cha CPP wakainakili kama ilivyo kwakuondoa jina cpp tu na kuweka Tanu. Katiba hiyo ndio hii inayotumiwa na ccm leo ambayo imekuwa ikiboreshwa tu miaka baada ya miaka, na katiba hii ndio iliyounda katiba ya nchi ya Tanzania hii ya 1977.
Vivyo hivyo TANU na KANU ambapo makamanda na makomred walikuwa wakiazima ujuzi na mapambano katika uwanja wa vita.
TANU chini ya rais wake Julius Nyerere iliwahi kuwatuma Bibi Titi Mohame na Mzee Tambaza kwenda Kenya kuwasaidia KANU iliyokuwa chini ya Kenyatta na Tom Mboya.
Mpaka leo wakolo hawa wapya weusi wanaoitwa vyama vya ukombozi wanashirikiana, yanayotokea Rwanda, Burundi, na Afrika kwa ujumla yote yana baraka za Tanzania. Yani ccm haiumizwi hata chembe... Demokrasia kwa ccm ya Magufuli ni anasa kwa Taifa.
Na Yericko Nyerere