Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Nimekua nikifuatilia mijadala ya bunge Hili la bajeti 2016 /17.Michango mbali mbali inatolewa na wabunge wa pande zote mbili, yaani wa chama tawala na wapinzani.Nataka nijikite kwa wabunge wa upinzani kwa kuwapa ushauri ambao si sheria na kama si sheria basi hawalazimishwi kuufuata.
Rais Magufuli baada ya kushika hatamu za uongozi alijitanabaisha ni tanzania ipi anayoitarajia kama kiongozi mkuu mwenye dhamana ya nchi.Alianza kwa kusafisha uozo serikalini ambao mliupigia kelele nyingi sana awamu ya nne ya mheshimiwa Jakaya kikwete.
Ameongeza makusanyo ya kodi kwa kuwabana wakwepa kodi, amebana matumizi yasiyo muhimu ya serikali pia amerudisha nidhamu ya watumishi wa umma.Sasa kwa kiasi flani ofisi za umma zinahudumia bila mizengo na hakuna njoo kesho kama zamani.
Haya yote mmeyapigia kelele sana hivyo nilitegemea mumuunge mkono kwa kutekeleza ilani ya chama chenu.Lakini sasa mnapinga Rais Magufuli kutumbua majipu, kifupi mnapingana na ilani yenu kwa kua wakati anaanza kazi hii baadhi ya viongozi wa upinzani walijitokeza hadharani na kusema anatekeleza ilani ya UKAWA.
Kuanza kupambana na Rais Magufuli kuhusiana na utumbuaji wa majipu kwa kumpangia nini afanye ili mfurahi si Sawa kabisa kwani anautaratibu aliojipangia wa kufanya kazi zake especially utumbuaji majipu.
Amesema haijalishi ni wapinzani au wana CCM, atadili nao, ni suala la kumpa muda.
Nashauri wapinzani kwa nia njema tusaidie juhudi hizi za Rais Magufuli kulikwamua taifa kwa kuleta michango mbadala bora kabisa kwa serikali ili ifanye vyema katika kustawisha taifa letu.Siasa za matukio tusizipe nafasi kwa sasa.Rais kaonyesha njia hatuna budi kumsapoti.
Vinginevyo wananchi wataanza kupoteza imani na siasa zinazofanyika nchini kwa kuona wanalaghaiwa na wanasiasa kwa wao kutumika ka ngazi ya wanasiasa kufikia malengo yao binafsi.
Ni mtizamo tu!