Wapingaji wa Rais Magufuli kuelekea 2025 wanafifia

Wapingaji wa Rais Magufuli kuelekea 2025 wanafifia

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
8,057
Reaction score
20,164
Amani iwe nanyi.

Rais Magufuli ambaye Tanzania na dunia kwa ujumla imemjua na kumwogopa kama rais mwenye kasi zaidi ametoboa siri ya mafanikio yake.

Rais Magufuli amesema katika safari yake ya mafanikio kisiasa tangu kuanza mpaka leo, wote waliojaribu kumkwamisha walikwama wao! Hali hiyo ilidhihiri kwenye wizara zote alizopita na hadi Sasa ni rais wa Tanzania.

Akiwa rais wa awamu ya tano wafuatao walijaribu kumkwamisha wakaishia kukwama wao kwa aibu kubwa.

1. Mange Kimambi
Huyu alishambulia sana mwanzo wa utawala wa rais Magufuli. Alitoa matusi ya kila aina na mwishoni akaitisha maandamano nchi nzima aliyopanga yafanyike siku ya muungano, yaani April 26! Matokeo yake aliishia kuandamana mwenyewe akielekea kwenye ubalozi huko Marekani, huku watanzania wakimpuuza na kuendelea kuchapa kazi. Tangu siku hiyo Mange Kimambi akafutika na akamwacha Rais Magufuli akiendelea kupeta kwa kuwaletea maendeleo Watanzania.

2. Tundu Lissu
Huyu nae amefutika tarehe 28/10/2020 baada ya kujaribu kwa miaka 3 mfululizo kukamisha juhudi za rais Magufuli.
Amezunguka duniani kote akimtukana rais Magufuli na Tanzania kwa ujumla lakini katikati ya matusi yake bank ya dunia ikatangaza Tanzania imeingia uchumi wa kati!

3. Godbless Lema
Huyu alikuwa mbunge wa Arusha akalipwa na mabeberu kumchafua rais Magufuli hadi akafikia hatua ya kuitangazia dunia kwamba ana ndoto ameoteshwa kuhusu rais Magufuli. Godbless Lema amefutika tarehe 10/12/2020 baada ya kutangazwa kuwa mkimbizi wa Canada; Lema licha ya kuwa mbunge kwa miaka kumi lakini sasa anaenda kuishi kambini kama wale wakimbizi wa Burundi wanavyoishi kule Kigoma!

4. Freeman Mbowe
Huyu amefutika kwa aibu kubwa. Chadema ilikuwa na wabunge zaidi ya 100 bungeni, leo hii ina mbunge mmoja tu!

5. Bernard Membe
Alijiaminisha ni kachero mbobezi mzee wa kazi na bata na akaahidi atamkwamisha na kumgaragaza vibaya Rais Magufuli kwenye uchaguzi mkuu wa October 28 mwaka huu, matokeo yake amegaragzwa yeye kwa kukataliwa na hata watu wa Lindi na hatainuka tena!
 
Nguvu za maraisi wa CCM zinaishia kwenye Uchaguzi wao wa mwisho ndani ya chama hapo mitandao hujengwa na yeye hitengwa na mitandao husika. Wakati itaamua ila hana nguvu tena hawezi manisha mambo mapya na kiyasimamia Maisha.

Kawanunulia nyumba mahawala zake kama Kajala wa cabins pale Bamaga

Kajinunulia na kujinafsisha nyumba kule area D Dodoma

Kamuuzia nyumba mdogo wake Musa Afu anajidai mzalendo?
 
Sio kufifia tu mkuu, hawapo kabsa.. nasikia mzee wa tungi na watoto wazuri kafungua m pesa!
 
Tengenezeni mada za kuunganisha Taifa hili. Kwa mtu alieshinda Uchaguzi iwe kwa giliba au ukweli huu sio wakat wa kuandika mada hizi. Andikeni Sera na mikakati ya kuikomboa nchi katika maadui wale manne wa maendeleo ambao ni ujinga ,umaskini na Ubaguzi wa itikadi za vyama. Nk.
 
Mkuu kwa sasa, waimba pambio na wakosoaji wana hali sawa tu, maana cement wananunua bei moja.
 
1.TUNDU LISSU NA BEN MEMBE
Hawa ni watu ambao kiukweli hawakuwa na haiba ya uongozi hawa watu ndiyo ambao wameviangusha vyama vyao na walijiona wao kuwa ni new political figure katika Tanzania ya Magufuli. Leo watu hawa wamekua ni wa watu wa kutapatapa kama mfamaji Wazungu ambao Lissu alitegemea watamsapoti wako wapi?

Leo ACT Wazalendo wakowapi? Leo ACT wamekubali kuyamariza na wamefunga ndoa na CCM chama dume . Leo Lissu hana hoja za kuwaambia watanzania,Ben nae leo atawaambia nini watanzania,Mange nae atawaambia nini watanzania.Ushauli wangu kwa hawa watu waje kuwaomba watanzania radhi kwani watanzania ni wakarimu watawasamehe
 
1.TUNDU LISU NA BEN MEMBE
Hawa ni watu ambao kiukweli hawakuwa na aiba ya uongozi hawa watu ndiyo ambao wameviangusha vyama vyao na walijiona wao kuwa ni new political figure katika Tanzania ya Magufuli.Leo watu hawa wamekua ni wa watu wa kutapatapa kama mfamaji wazungu ambao Lissu alitegemea watamsapoti wako wapi?
Leo ACT wazalendo wakowapi? Leo ACT wamekubali kuyamariza na wamefunga ndoa na CCM chama dume .Leo LISU hana hoja za kuwaambia watanzania,Ben nae leo atawaambia nini watanzania,Mange nae atawaambia nini watanzania.Ushauli wangu kwa hawa watu waje kuwaomba watanzania radhi kwani watanzania ni wakarimu watawasamehe
Umewashauri vizuri
 
Tengenezen mada za kuunganisha Taifa hili. Kwa mtu alieshinda uchaguzi iwe kwa giliba au ukweli huu sio wakat wa kuandika mada hizi. Andikeni Sera na mikakati ya kuikomboa nchi katika maadui wale manne wa maendeleo ambao ni ujinga ,umaskini na Ubaguzi wa itikadi za vyama. Nk.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Usaliti na ukuwadi wa mabeberu nalo ni janga kwa taifa
 
Back
Top Bottom