Kama inavyoeleweka chama kinachoongoza Serikali kinapata kura nyingi kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma.
Na zipo kata nyingi katika Jimbo la Dodoma mjini.
Na Kama utafuatilia kata zinazoongoza kwa kukipa kura chama tawala huto acha kuitaja kata ya Chamwino iliyopo Mjini kati,
Hii ni kata kongwe sana, lakini ni kata ambayo hutengwa katika miradi Mbalimbali inayo tekelezwa na Serekali.
Miundo mbinu ya mitaa ya Chamwino mjini kati ni mibovu! hususan barabara,Mifereji ya kupitisha Maji ya mvua na Mifumo ya kisafirisha maji taka!.
BARABARA: ipo barabara moja tu ya kiwango cha lami inayopita katika kata hii ikitokea njia panda ya Area C kuelekea chang'ombe ambayo inapita mbele ya soko la Matunda la Bonanza,lakini barabara za mitaa zote ni hovyo na hazifanyiwi matengenezo yoyote na hivyo imekuwa ni kero ya Muda mrefu kwa wakazi wa kata hiyo.
MIFEREJI YA MAJI YA MVUA: Wakati wa kipindi cha awamu ya Kwanza na ya pili katika uongozi wa nchi hii,Miundo mbinu ya Mifereji ya kupitishia Maji ya mvua na Makaravati ya mtaa kwa mtaa yalikuwa yanafanyiwa usafi kila mara.
Leo ukipita mitaa ya Chamwino kati huoni mifereji ya Maji Wala Makaravati yaliyo wekwa zamani, Makaravati yote yamefukiwa chini na Mitaro yote imejifukia kiasi kwamba Maji ya Mvua yanatembea juu ya Barabara na kuziharibu.
Mitaa ya Chamwino Mjini kati imepangika vizuri kwa Ramani hivyo hakuna kisingizio cha kuto weka barabar nzuri na mifereji,upana wa barabara unaonekana wazi sijui tatizo liko wapi!
Wakati wa Masika barabara hukatika vibaya na hivyo kuwa ni kero ya miaka nenda rudi.
Miaka michache iliyo pita serekali ilikuwa ikileta magreda kuzikwangua barabara chache na kuweka vifusi vya changarawe! katika barabara ambazo hazina karavati Wala mifereji ya kupitishia Maji ya mvua
kinacho tokea ni kifusi kusafirishwa na maji ya Mvua kila kinapo wekwa,Sijui serekali haiioni hasara hii au vipi.
Kwa kuwa mtandao huu wa Jamii unatembelewa na viongozi wengi wadau wa kata ya Chamwino mjini kati wameona ni njia bora kufikisha kilio chao cha Muda mrefu!
Wanachoomba wakazi wa kata ya chamwino mjini kati ni kuwa Kama Serekali haina mpango wa kuziwekea lami barabara za mitaa hiyo!
Basi waweke angalau miundombinu bora ya Mifereji ya kupitishia Maji ya Mvua na Makaravati yanayo unga mtaa kwa mtaa,
Kwa bahati nzuri Mfereji mkuu wa kusafirisha Maji yote ya mji upo jirani kabisa na kata hiyo! Lakini huwezi kuamini Maji ya Mvua hutuama katika eneo lisilo zidi mita 200 kutoka mahali ambapo mfereji mkuu unapita .hivyo hakuna kisingizio chochote cha Maji ya Mvua kukosa muelekeo.
Kuna barabara inayo pita mbele ya Hoteli inayo itwa AVE MARIA ipo nyuma ya Bustani ya mpya ya CHINANGALI PARK. ni barabara Muhimu na inatumiwa na watu wengi na hata barabara kuu ya Arusha inapokuwa ina changamoto ya misafara ya viongozi watu wengi huitumia barabara hiyo ya nyuma!
Lakini barabari hiyo bado ni ya Vumbi na huweka mabwawa makubwa ya Maji wakati wa Masika na wakati mfereji Mkuu wa kupitisha Maji ya Mvua upo umbali usio zidi mita 200.
Hebu serekali iangalie umuhimu wa barabara hiyo na ichukue hatua.
MAJI TAKA: Maji taka ni kero ya Muda mrefu ya wakazi wa kata ya Chamwino mjini kati, Mabomba makubwa ya kusafirisha Maji taka yaliyo jengwa tangu wakati wa Mwalimu yapo jirani kabisa na kata hiyo.
Lakini kwa sababu ya mipango mibovu ya DUWASA ya kuruhusu watu kujiungia mabomba ya kusafirisha Maji taka bila utaalamu imepelekea mabomba ya mitaani kuziba mara kwa Mara na kutiririsha maji taka nje kwenye makazi ya watu na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wa kata hiyo.
Wakati wa kampeni tuliambiwa serekali ina mpango kabambe wa kurekebisha mifumo ya maji taka katika kata hiyo!
Lakini hadi leo hakuna dalili ya mpango kabambe!
Hivyo wakazi wa chamwino mjini kati wanaomba serekali iliangalie suala Hilo na kero hizo zote zitafutiwe ufumbuzi wa haraka.
Wakazi wa chamwino mjini kati wanasikitishwa kuona kwamba Serekali inawekeza pesa nyingi kwenye maeneo mapya na kuwasahau wapiga kura wao Muhimu.
Naomba kuwasilisha.