Wachina wana bei reasonable kulingana na ubora wa kazi zao... Hawako cheap, na sio expensive ukilinganisha na Muda wa kazi, less longo longo na quality ya kazi yenyewe.. Siwapigii debe ila ukipeleka gari pale utajua nini nasema... kuhusu bei, Mimi kuna mtu alinigonga nyuma, bumper likachanika kabisa na kubonyea vibaya na mlango wa nyuma ukabonyea kabisa, wakataka 380,000 kwa kazi ya siku mbili na matokeo yake ni mazuri sana, yaani hakuna anayejua kama gari iligongwa kama sikumwambia, ni kama imekuja jana kutoka japan, Pia bro wangu aligongwa na tiper, bumper ya mbele iling'oka yote na taa zikavunjia, wachina walitaka 250,000 kwa kazi nzima na sasa hivi ukiliona gari utadhani limenunuliwa mwezi huu wakati lina mwaka sasa.. kwahiyo jamaa mi naona wana bei za kawaida tu kulingana na ubora wa kazi zao.... Mafundi wa mtaani ukilaza gari kwao hesabu maumivu, ukishamaliza kazi ya rangi, matatizo ya engine nk yanaanza, huku wanatengeneza na kule kuna wezi wanalihujumu gari lako... Na huna ushahidi wa kumfunga mtu... Wachina ukienda pale, wana form yao ya kukagua gari, wanalicheki kila kitu na wanarecord kila kilichopo kwenye hiyo form na ukija kulichukua wanapitia tena kucheki kila kitu kipo...
Ni mtazamo tu.