Wapi wameshinda cuf | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapi wameshinda cuf

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ami, Nov 2, 2010.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mbona sijaona mahala CUF imeshinda ubunge bara kama wenzao akina CHADEMA hata nccr mageuzi.Au nimepitiwa tu.
  Nilisikia Mbeya,Mtwara halafu Tanga na bUKOBA,lakini sijaona !.
   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lindi Mjini, japo sina hakika kama wameishatangaza rasmi.
   
 3. F

  Fikra Pevu Senior Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hamna mahali wameshinda mpaka sasa.
   
 4. M

  Mwera JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Cuf wameshinda lindi mjini nec wametangaza rasmi,na zenj wamepata majimbo 22 jumla mpk sasa wana wabunge 23 safi, wakubaliane na chadema waungane bungeni waipeleke puta ccm na mafisadi wake,aluta continua.
   
 5. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  CUF hawawezi kushinda bara kwa kuwa ni chama cha uchaguzi na si chama cha siasa.CUF wao baada ya uchaguzi huwa wanajisahau hawazunguki mikoani kujenga chama,huku bara si kama Pemba ,huku chama kilicho karibu na wananchi ndicho kinachoweza kushinda viti vya ubunge na udiwani.


  Hii inaonesha kuwa kwa miaka karibuni 15 Prof.Lipumba aliyokaa madarakani kama mwenyekiti ameshindwa kukiuza chama cha CUF kwa wananchi.

  Mimi nawashukuru sana CHADEMA chini ya uongozi wa MBOWE,SLAA,ZITTO NA MNYIKA wamefanikiwa kukiuza chama kwa wananchi kupitia Operasheni Sangara na wameweza kuonesha kuwa CHADEMA si chama cha maeneo fulani kama kilivyo CUF(Pemba) BALI cha KITAIFA
   
 6. M

  Mwera JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dafirs hapo umenena cuf wamejisahau wamekaa zenj tu bara wanasubir uchaguzi ndio wanaamka,sasa wamevuna walichopanda,ila cuf wenyewe wanadai wamelishinda lindimjini,lindivijijini,kigamböni,temeke,tangamjini,lushoto,uyui,na data wanazo zavituoni,ila wanadai ccm imechakachua matokeo,
   
 7. czar

  czar JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 8. Abdallah M. Nassor

  Abdallah M. Nassor Verified User

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 592
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 180
  Kama CUF ni chama cha Pemba sawa, nambie sasa kama CHADEMA sio chama cha Bara. Maana Pemba hawana ofisi wala hawakuja kukampeni, kwani Pemba sio Tanzania? Acheni maneno ya vijiweni nyie.
   
 9. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hizo data zina dalili ya ukweli.Kuhusu kujitangaza hakuna kama CUF.Tatizo lililopo chaguzi Tanzania na Afrika ni kuppotezeana muda tu.uwamuzi huchukuliwa mezani.
  Watu wa CHADEMA mukiwa na msimamo kwamba CUF hawajitangazi basi mukubali kuwa uchaguzi uliomalizika na matokeo yanayotangazwa ndio ukweli,hivyo kaeni kimya.
   
 10. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  JAMAN TUWE MAKIINI ILI JF IWE JUU, TUSIKURUPUKE KUTOA TAARifA kAmA hujvERIFY.
  MWEnzetU KAULIZA CUF WAMESHINDA WAPI BARA?
  JIBU SahiHI:
  CUF wako Lindi Mjini na KILWA KUSINI TU. HIVYO WANAMAJIMBO MAWILI HUKU BARA
   
 11. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa kila wakipata nafasi ya kuikandamiza CUF madongo basi hawachelewi kufanya hivyo. Huu ni uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. CUF imenyakua viti vingi tu vya udiwani huku Bara na hivyo kufanya hayo madai ya kuwa CUF ni chama cha wakati wa uchaguzi ni za uongo, uzushi na fitna za kike. Mwaka jana (miezi 12 tu iliyopita) ulifanyika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji Tanzania Bara tu na CUF ilishika nafasi ya pili baada ya CCM ikifuatiwa kwa mbali na Chadema. Hiyo nayo inathibitisha kuwa anayedai kuwa CUF ni chama cha wakati wa uchaguzi tu kuonekana ni mbumbumbu na asiyejua mambo ya upinzani. Sana sana ni mtu wa juzi alitoka CCM.

  Kilichofanyika uchaguzi huu ni yale maneno ya Prof. Lipumba kuwa "mapapa, nyangumi, na masangara yanashirikiana kuihujumu CUF".
   
Loading...