Wapi tunakosea vijana mpaka tunashindwa maisha Mazuri?

Wapi tunakosea vijana mpaka tunashindwa maisha Mazuri?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,678
Reaction score
5,166
Habari wanajukwaa!!

Maisha yanazidi kuendelea huku miaka ya kuishi ikiendelea kuisha bado nipo katika tafakari nzito Juu ya ombwe la vijana kukata tamaa kabisa ya kufanikiwa kimaisha.

Hali ngumu ya maisha hupelekea vijana wajiingize kwenye matumizi mabaya ya madawa ya kulevya,bangi na wizi.

Mimi ni mmoja ya wahanga wa hali hiyo lakin sijafikia huko lakin jana usiku nimejiuliza sana hivi ni kweli kijana mwenye upeo na maono unashindwa kupata pesa kwelii??

naomba niwasilishe kwenu hoja hii.
 
Pesa kila mmoja anaweza kupata aliye na upeo au ambaye hana suala kubwa linakuja kwenye matumizi ya hiyo pesa, wategemezi wa huyo mtu n.k

Kila mtu anapata pesa bwana.
 
Pesa kila mmoja anaweza kupata aliye na upeo au ambaye hana suala kubwa linakuja kwenye matumizi ya hiyo pesa, wategemezi wa huyo mtu n.k

Kila mtu anapata pesa bwana.
Bado hujakutana na vijana wengine wenye hali hiyo Kaka.
 
tunakosea kupotozea mda mwingi kufanya mambo yasiyo na manufaa kwetu mfano kukaa vijiweni kutwa nzima na kuomba pesa kwa ndugu huku hatuna maono ya kuwekeza na kujitegemea kiuchumi, huyo ndo mchawi wetu mkubwa.
 
Anaishi vp km hana pesa? Pesa ndio maisha uwe unaomba, tafuta au okota ili mradi Kila MTU anapata pesa
 
Mwenye akili ,upeo na juhudi hasa kijana huwezi kufeli jumla maisha,may be unaweza ukachelewa ila siamini kufail jumla kimaisha japokuwa serikali za kiafrika sio supportive
 
Me nadhani tatizo ni kuwa tunataka mafanikio ya haraka haraka, mtu unafanya jambo kidogo tu ukiona 'halikulipi' unaliwacha.
Kijana ukikaa unatamani kuwa kama mzee mengi ila cha ajabu hutaki kupitia yale aliyopitia yeye, tunataka mafanikio ya kulala maskini na kuamka tajiri.

Kwa kifupi kabisa, TUNATUMIA MUDA MWINGI KUWAZA KUWA NA MAFANIKIO KULIKO MUDA WA KUFANYA KAZI KUYAPATA HAYO MAFANIKIO YENYEWE.
 
Back
Top Bottom