Kipindi cha "This week in perspective" kilichokuwa kinaendeshwa na Adam Simbeye na kuoneshwa kila ijumaa saa 2.30 usiku kilikuwa na changamoto kubwa kwenye uendeshaji wake. Kwa kuwa kilikuwa kinaendeshwa kwa lugha ya kiingereza, kuwapata washiriki ilikuwa kazi kubwa mno.Simbeye akipeleka mwaliko kwa mtu kushiriki mara nyingi mtu aliyealikwa hutoa visingizio kibao kukwepa kuhudhuria.Hali hii ilimfanya Simbeye kushindwa kuendesha kipindi hivyo akakifutilia mbali.