Wapi naweza kupata mkopo kausha damu

Wapi naweza kupata mkopo kausha damu

Status
Not open for further replies.

Deleted_account

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2008
Posts
3,385
Reaction score
3,702
Wadau habari,

Hali imekuwa mbaya kiuchumi nimepata emergency, wapi naweza kupata wanaokopesha hao wanaita kausha damu nikope kwa riba hadi mwisho wa mwezi tu.

Wezi wamenikombea vitu ndani nimebaki mweupe, hata mtu binafsi kama anaweza kunisaidia.

Asanteni, nipo Dar.
 
Asanteni, nipo dar.
Unafahamu maana ya hilo neno "KAUSHA DAMU" ulilolitumia kwenye title?
 
Hapo kwenye bondi ndio changamoto maana wamenikombea hadi vile vichache nilivyokuwa navyo, ila ni muajiriwa na mtu anaweza kuja hadi ninapofanyia kazi na nikampa na vithibitisho vingine.

Kiasi ni laki 1 tu, riba ataniambia yeye. Narudisha tar 25
Kama kweli umeajiriwa na huwezi kukopeshwa laki moja na muajiri wako basi jipange utafute shughuri nyingine ya kufanya, huna ajira una kibarua tu.
 
Hapo kwenye bondi ndio changamoto maana wamenikombea hadi vile vichache nilivyokuwa navyo, ila ni muajiriwa na mtu anaweza kuja hadi ninapofanyia kazi na nikampa na vithibitisho vingine.

Kiasi ni laki 1 tu, riba ataniambia yeye. Narudisha tar 25
Laki moja umekosa wa kukopa hapo ofisini wala mtaani pako? Wewe ni tapeli au mdhulumaji
 
Hapo kwenye bondi ndio changamoto maana wamenikombea hadi vile vichache nilivyokuwa navyo, ila ni muajiriwa na mtu anaweza kuja hadi ninapofanyia kazi na nikampa na vithibitisho vingine.

Kiasi ni laki 1 tu, riba ataniambia yeye. Narudisha tar 25
Dah asee nilijua hata unataka hela kumbe hutaki. Laki ndio uandike uzi?
 
Kama ni mfanyakazi, nenda Ultimate hawahitaji dhamana bali salary slip tatu za miezi ya hivi karibuni, mshahara uwe unapita Bank ya NMB, CRDB au NBC pamoja na Bank Statement ya miezi mitatu ya hivi karibuni.

Wanakupa mpaka 25% ya take home yako na unapewa siku hiyo hiyo.

Bank nimekutajia hizo ila inawzekana na Bank zingine zinahusika.

Kupata namba zao, google Ultimate Finance utapata mawasiliano yao.

Pole sana ndugu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom