Kwa Dar yanauzwa maeneo mengi tu ila ili usipoteze muda wako kwa kuzunguka sana nenda mitaa iliyopo Kariakoo hususani Livingstone, Swahili au mitaa mingine kuanzia barabara ya Uhuru kuekekea usawa wa Gerezani kuna maduka mengi na yenye ubora na bei tofauti. Pia kuna wale wengine ambao wanauza overalls, reflective jackets na safety gears zingine ambazo zinakuwa zimechapishwa kabisa jina au nembo ya kampuni japo gharama zao uwa zipo juu zaidi.