Wapi napata mtaalamu wa magonjwa ya ngozi ili nipate msaada

shamajengo

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
1,217
1,431
Habari zenu wanajf wenzangu, ashukuriwe Mungu kwa kutujalia uzima siku ya leo, tukumbuke kuwaombea wale waliopo mahospitali na majumbani kwa maradhi mbalimbali wakaweze kupona. Lakini tuwaombee wapumzike kwa amani wale ambao Mungu amewatwaa Siku ya leo nasi tuseme amina.

Wakuu ninashida ya ngozi nimeenda hospital mara kadhaa ila bado tatizo haliishi huku majibu yakiwa hayaonyeshi tatizo zaidi ya kupewa anti allergy plus anti fungal.

Yapata miezi mitano na zaidi sasa vinanitokea vipele sehemu za mikononi hasa kati ya vidole vinawasha nikikamua vinatoa maji na hapo hupungua kuwasha kama siyo kuacha kabisa.

Lakini sehemu za mapaja na scrotum pia navyo ni hivyohivyo nimetumia dawa tofauti tofauti za fangus bado sipati majibu.

Kama kunayeyote mwenye kujua juu ya shida hii anisaidie au anifanyie msaada wa kujua wapi nitapata specialist wa ngozi ili nikapate Tiba....natanguliza shukrani

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wanajf wenzangu, ashukuriwe Mungu kwa kutujalia uzima siku ya leo, tukumbuke kuwaombea wale waliopo mahospitali na majumbani kwa maradhi mbalimbali wakaweze kupona. Lakini tuwaombee wapumzike kwa amani wale ambao Mungu amewatwaa Siku ya leo nasi tuseme amina.

Wakuu ninashida ya ngozi nimeenda hospital mara kadhaa ila bado tatizo haliishi huku majibu yakiwa hayaonyeshi tatizo zaidi ya kupewa anti allergy plus anti fungal...
Tafuta dawa inaitwa scaboma ndugu yangu vitakwisha
 
Habari zenu wanajf wenzangu, ashukuriwe Mungu kwa kutujalia uzima siku ya leo, tukumbuke kuwaombea wale waliopo mahospitali na majumbani kwa maradhi mbalimbali wakaweze kupona. Lakini tuwaombee wapumzike kwa amani wale ambao Mungu amewatwaa Siku ya leo nasi tuseme amina...
Usitumie antifungal pekee, tafuta dawa zenye mchanganyiko wa antifungal, antibiotic na antiallergy mfano Gentrisone ina gentamicine ,clotrimazole na betamethasone, the same to sonaderm nayo ina dawa tatu itakusaidia.

Pia huko sehemu za korodani tumia dawa pia ujitahidi usafi na kuvaa nguo zisizobana.
 
Mkuu pole sana kwa changamoto magonjwa ya ngozi yanahitaji utaalam wa hali ya juu kuyatibu kwa ufasaha nakushauri uende Regency Hospital kamuone Prof. Mgonda anaweza kukusaidia huyu jamaa ni fundi alinisaidia shida iliyonisumbia zaidi ya miaka sita.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani Nina tatizo la ngozi Naomba kujua Tiba yake ngozi Ina kakamaa miguu yote ilianza kidogo saiv naona inaongezeka

IMG-20210424-WA0029-01.jpeg
 
Back
Top Bottom