Mkuu yuko safarini akiongoza kamati yake ya Ulinzi na Usalama kutembelea balozi za Tanzania katika nchi tajiri (hakuna hata moja masikini), yeye anaongoza kamati iliyokwenda Canada, New York na Washington DC, na ameambatana na mkewe Regina Mumba Lowassa (si mbunge) na walinzi wawili na wamesafiri daraja la kwanza na yeye atakaa siku 21: wenzake wengine akiwamo Chiligati, Zungu, Anna Abdalah, Mohammed Seif Khatib watakaa siku 14 katika nchi za Ulaya na Asia, ziara ambayo imezua maswali mengi kuliko majibu. Bahati mbaya ameondoka Juni 26, siku ambayo kumetokea mambo ya aibu kwa Taifa letu. More to come, je, amekwenda kumchimba Membe? Je, amekwenda kufuatilia vijinsenti (yale madola Uswisi), ama wastaafu wamekimbia bajeti na wao kwenda kupumzika? Bejeti yao ya safari imetoka wapi? Ama ndio kuwahi kumalizia mabaki ya bajeti ya mwaka unaoisha wakwangue sizirudi?