Wapi kuna makosa kwenye elimu?

Obamaeli Rutajecha

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
230
274
Amani kwenu wakuu!

Ni muda mrefu katika sekta ya elimu kumekuwa na pande mbili zinazotoa huduma hiyo, yaani serikali kupitia shule na vyuo vyake na watu binafsi kupitia mashule na vyuo vyao.

Nimefikiria sana pamoja na uchunguzi wa muda mrefu na kuamua kuileta hoja yangu hii humu kunakojulikana kama nyumbani kwa wenye kufikiri vizuri.

Ngazi ya msingi na sekondari

Nafikiri wote humu ni mashahidi wa elimu itolewayo katika shule za serikali na ile inayotolewa katika shule binafsi na mtakuwa ama pamoja nami au kunikosoa pale nitakapokosea.

Shule binafsi za primary na secondary zinajitahidi sana katika kutoa elimu bora na sote ni mashahidi kwani hata tukiangalia performance yao katika matokeo ni nzuri na mara nyingi hushika nafasi kumi za mwanzo na kuzitupa mbali kabisa shule za serikali. Upande mwingine ni hizi shule za serikali zikitoa wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kutosha na huku wengi wakipata matokeo mabovu.

Ngazi ya elimu ya juu
Kwa hapa tunakunata na vyuo vinavyotoa elimu ya juu, na hapa kuna vyuo binafsi na vyuo vya serikali.
Tukiangalia hapa utagundua kuwa vyuo binafsi vimetupwa mbali sana kwa kutoa elimu bora na hata katika kuheshimika. Vyuo vya serikali vinazalisha wahitimu vichwa sana na hili sio siri hata ukijaribu kuchunguza utabaini huko maofisini. Lakini kwa upande wa vyuo binafsi wahitimu wake asilimia kubwa sio wa kuaminika na hawako vizuri kama wale wa vyuo vya serikali.

Sasa msingi wa hoja yangu ni huu hapa:

Ni wapi watoa huduma hii ya elimu kwa ngazi ya juu kupitia vyuo vyao binafsi wanakosea?

Ni kwanini vyuo vya serikali viko strong lakini shule zake hazipo strong?

Kwanini shule za private zinatoa elimu nzuri lakini ukija kwenye vyuo binafsi sio tishio kama shule hizo?


Tahadhari:
  • Ni vizuri sana ukaweka mahaba ya pale ulipopata elimu yako pembeni ili ujadili hoja vizuri.
  • Ni vyema pia ukaeleza madhaifu ya pale ulipojitwalia elimu yako kama ni public au private itasaidia kujua tatizo ni nini.

 
Back
Top Bottom