nzuri sanaNimefungua thread hii maalum kwa ajili wapenzi wa nyimbo za oldskool, miaka ya '90s kurudi nyuma. Unaruhusuwa kuomba wimbo wowote wa oldskool wa nje (sio bongo fleva), na tutaweka hapa. Hii ni kukumbushana enzi za mtaa wa mangoma (enzi za DJ JD, Fast Eddy, nk) na wengineo. Mwenye wimbo atatupia humu ili anaeutaka kupakua apakue. Kama kuna wimbo wa oldskool umeusaka kwa muda mrefu na hujaupata, basi hapa ndio mahali pake pa kuupata. Karibuni.
Naanza hivi