Wapenzi wa Gaming Pc & Building

Wapenzi wa Gaming Pc & Building

h120

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
2,545
Reaction score
3,367
Habari zenu wana tech,

Najua kuna wapenzi wengi wa gaming, kuna wale wa pc, consoles na pia hata kwenye smartphones wengine huburudika pia.

Leo ntawagusa zaidi wale wa PC, lengo kuu likiwa ni kupeana miongozo katika uundaji wa Gaming pc, najua kuna wengi hawajui wapi ka kuanzia na wapi pa kuishia, ila tutaeleza kidogo kidogo ili kupata ufahamu, miongozo yote twafahamu ipo mtandaoni ila wengine huona uvivu au kuhisi vitu hivo kwa mazingira yetu ni ngumu kuvifanikisha, ila kila kitu kinawezekana.

Changamoto katika uundaji wa gaming pc ni fedha tu, hichi ndicho kikwazo kikuu, maana sote tunajua vitu vizuri vina gharama, ila kama mfuko upo vizuri wala hamna ugumu wowote.

Hivi karibuni nimefanya custom build moja na nitatumia hiyo kama reference katika kuelezana.

Kabla ya hii mashine ya sasa nilikuwa natumia Dell hii:
Dell Optiplex 790
intel core i5 3.1Ghz (Second generation)
8GB RAM
1TB HDD (storage)
64GB SSD (OS) brand samsung
Zotac Geforce GTX 560 1GB

Hii niliiuza nadhani hata wengine mtakua mliona mabandiko ya hii mashine humu JF, niliamua kuuza kwasababu nilitaka kufanya upgrade. Niliuza mashine peke yake na Graphics card peke yake, hivyo nilikuwa na fungu la kuanzia katika mashine mpya nitakayo ijenga.

Manunuzi baadhi ya vitu nimefanya Ebay na vingine hapa hapa nyumbani TZ, sinta zungumzia jinsi ya kufanya manunuzi ebay kwasababu tayari zipo thread zimechambua na kuelezea A to Z kwa newbies.

Kitu cha kwanza kabisa kutafuta ilikuwa ni processor, unaweza ukauliza kwanini processor, kwa upande wangu processor ilikuwa ni muhimu kuitafuta kwanza kwasababu, options za kupata motherboard itakayo support processor husika ilikuwa ni rahisi, kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba ningepata motherboard kwanza ningesumbuka kupata processor ya hiyo motherboard, ila ningepata processor kwanza nisingesumbuka kupata motherboard ya hiyo processor.

Motherboard huendana na processor huwezi chukua processor aina fulani ukaiweka kwa motherboard fulani ikafanya kazi unless ziwe compatible, (Na compatibility hatuangalii ufanano wa pin za processor, pin zaweza fanana na zisiwe compatible, mafundi wetu bongo wengi huangalia ufanano ila si sahihi kufanya hivo unatakiwa kuangalia specs za processor au motherboard husika) Ipo thread Chief-Mkwawa amezichambua bila shaka.

Nilinunua processor kupitia humuhumu jamvini kwa nixp ni intel core i5 3.2Ghz Fourth generation, mnaweza kumcheki anauza uza parts za pc, cards n etc.
1398462984Procesador_Intel_Core_i5-4570-1.jpg

Baada ya kupata processor motherboard haikuwa shida sana kuipata, Hivyo niliagiza motherboard kupitia Ebay, Motherboard zipo aina nyingi na zenye specs tofauti tofauti chakuangalia kwanza ni compatibility halafu ndio urukie kwenye features na korokoro nyingine, kwa processor niliyokuwa nayo ya Haswell(Fourth generation) nilihitaji motheboard ya socket LGA 1150 (hii ina support 4th na 5th generation intel processors)

Model niliyochukua ni GIGABYTE Z97X-SLI LGA1150 i3/i5/i7 ATX
Gharama ni $105.62 + $26.39 shipping
IMG-20160803-WA0004.jpg
IMG-20160803-WA0005.jpg
IMG-20160803-WA0006.jpg
IMG-20160803-WA0009.jpg

Graphics card
Niliagiza MSI GTX 960 2gb, nilinunua 2 moja niliuza
Gharama $165 + $40 shipping (kwa moja)
IMG-20160713-WA0003.jpg
IMG-20160713-WA0002.jpg

Power supply
Hii niliagiza mwaka jana, OCZ ModXStream Pro 500 W 80+ efficiency
Gharama $60 (free shipping)
IMG_1006.JPG
IMG_1007.JPG
IMG_1011.JPG
IMG_1021.JPG
IMG_1022.JPG

Case/Chasis
Hili ni jumba na kuhidhi motherboard na makorokoro yote, nilitafuta case itakayoendana na motherboard yangu, case zipo aina nyingi na zina ukubwa tofauti, chasis nzuri ni za hp kwasababu zina support ATX motherboard nyingi tofauti na za dell, nilinunua chasis ya HP XW 4300, nimefanya modification chache kwenye switch na motherboard backet ili motherboard yangu ikae vizuri.

Gharama 45,000 (Bei hii ni kubwa sana kwa PC case ila maeneo nilipo nilikuwa sina alternative option, bei za case ni 10,000-20,000 zisizidi hapo)
1.jpg
we.jpg

CPU heat sink
Arctic Cooling Freezer 7 Pro Rev 2 CPU Cooler
Hii ni cooler ya kupooza processor, nayo nimefanya kuagiza yenye ubora zaidi
Gharama $37 pamoja na shipping (Hii bado haijafika)
pix.jpg

HDD, RAM,
Nilikuwa na reserve HDD ya 500GB na pia nimepata SSD ya 120GB kwa mdau wangu mmoja, pia kwa sasa RAM ninazo ya 4GB soon nitaongeza nataka niwe na 8GB yatosha.

Hapo ndipo nimefikia kwa sasa nangoja cooler ifike niwashe Mashine,
Total cost $493.25

****UPDATE****
CPU fan imefika
IMG-20160831-WA0000.jpg
IMG-20160831-WA0001.jpg

Karibuni kwa maswali na michango zaidi.
 
Attachments

  • IMG-20160713-WA0001.jpg
    IMG-20160713-WA0001.jpg
    74.2 KB · Views: 166
Build iko poa sana, hapo unapelaka games nyingi kwenye 1080p Ultra 60fps, ila kama unataka ucheze kwa 1440p hiyo gtx960 umeumia 60fps hufikishi kwa AAA games, hiyo powersupply vipi, naona kama umeinyima sana hiyo PC, gtx960 zinakunywa umeme wa kutosha, malizia cover tu maana hilo la hp linafanya machine ionekane ka pentium 4. Overall build kali, hapo utaenjoy performance kwa muda mrefu. Ukiingia kwenye VR itabidi utupe hiyo 960
 
Build iko poa sana, hapo unapelaka games nyingi kwenye 1080p Ulta 60fps, ila kama unataka ucheze kwa 1440p hiyo gtx960 umeumia 60fps hufikishi kwa AAA games, hiyo powersupply vipi, naona kama umeinyima sana hiyo PC, gtx960 zinakunywa umeme wa kutosha, malizia cover tu maana hilo la hp linafanya machine ionekane ka pentium 4. Overall build kali, hapo utaenjoy performance kwa muda mrefu. Ukiingia kwenye VR itabidi utupe hiyo 960
Monitor ninayotumia resolution max 1080 kwa hiyo hata card ingekuwawa ina push 1440 au 4k ni useless. Kuhusu case kupata case nzuri ni changamoto kidogo, ila kama ikipatikana nzuri ipo ndani ya bajeti yangu, i will take it.
 
build nzuri mkuu imebalance cpu/gpu wise, ila kwenye motherboard hapo unaplan ya ku overclock baadae? sababu kunakuwa na board za H na B series ambazo ni rahisi zaidi ila hazina feature za ku overclock kwa mimi naona kama ni nzuri zaidi kwenye cpu ambazo zipo locked.
 
Hii motherboard inatumia Z97 chipset na pia ina support overclocking
Kama walivyo indicate intel kwenye specs za hii chipset
5rt.JPG

Na hii ni tofauti kati ya Z97 na H97
Capturert.JPG

Overclocking sina mpango huo, maana processor niliyonayo ipo locked na pia cooler niliyo order sio friendly sana na overclocking.
 
build nzuri mkuu imebalance cpu/gpu wise, ila kwenye motherboard hapo unaplan ya ku overclock baadae? sababu kunakuwa na board za H na B series ambazo ni rahisi zaidi ila hazina feature za ku overclock kwa mimi naona kama ni nzuri zaidi kwenye cpu ambazo zipo locked.
Yap ni kweli H na B series ni cheap ila nilipenda hii sababu iko na features nyingi.
 
This is my beast, ni muda kidogo toka nimemuweka pamoja ila hajawahi niangusha.
Motherboard natumia kama yako Gigabyte Z97, CPU ni i7-4790, 8GB Kingston Hyperx Fury, 1TB HDD, 256GB Samsung 850-EVO SSD, hiyo display nilinunua cheaper kutoka kwa wachina 27" 2560x1440, GPU kwa sasa natumia GTX 1070 hii inapush QHD fps za kutosha, kama Overwatch haishuki 90FPS kwa Ultra Settings. Cover ni Corsair Obsidian series, feni sikununua extra, hizo zinawaka hapo zilikuja na cover sioni haja ya kununua nyingine coz sina hata mpango ya ku~overclock, it works smoothly. Imebaki kuvuta tu Oculus Rift nimalize na Virtual Reality moja kwa moja.

View attachment 390403
build imetulia mkuu
 
Beast
 
ujamaliza tu kuunda mashine mkuu
Yap mkuu, bado kidogo sana, cooler niliyoagiza ilikuwa na shida hawakuweza kuituma, nilifanya kwanza process za refund ndipo nikaaagiza nyingine, hiyo ndiyo imenichelewesha.
Ngoja niweke picha kidogo uone ilipofikia, ila picha quality si nzuri ntakuja kuweka picha zenye quality bdae.
IMG_20160830_162347.jpg
IMG_20160830_162359.jpg
IMG_20160830_162656.jpg
IMG_20160830_162701.jpg
IMG_20160830_162715.jpg
IMG_20160830_162813.jpg
IMG_20160830_162921.jpg
IMG_20160830_163106.jpg
 
Yap mkuu, bado kidogo sana, cooler niliyoagiza ilikuwa na shida hawakuweza kuituma, nilifanya kwanza process za refund ndipo nikaaagiza nyingine, hiyo ndiyo imenichelewesha.
Ngoja niweke picha kidogo uone ilipofikia, ila picha quality si nzuri ntakuja kuweka picha zenye quality bdae.
View attachment 390437 View attachment 390439 View attachment 390441 View attachment 390443 View attachment 390446 View attachment 390447 View attachment 390450 View attachment 390451
Jitahidi upate na case nzuri kaka eBay huwa naona kuna cheap case hopefully it will be ndani ya bajeti yako far from that Build imetulia mbaya yani huyo ni "Beast in the Cage akiachiliwa ataleta hatari" , me Tanesco walichoma card yangu nataka nianze na moja halafu sijaona bei ya processor hapo juu.
 
Ni kweli case/chasis kwa ebay zipo nyingi tu bei rahisi, tatizo linakuja kwenye shipping, unaweza kuta linauzwa let's say $30 ila shipping $250 hapo ndipo tatizo linakuja. Ila ukiachana na good looking nilihitaji case yenye nafasi ya kutosha na hapo hili la hp nililotumia limekidhi.
 
Pamoja mkuu, so Processor ulichukua kwa ngapi hiyo?
 
Pamoja mkuu, so Processor ulichukua kwa ngapi hiyo?
Kuanzia 100k na kuendelea inategemea maongezi na muuzaji pia generation na specs za cpu husika.
 
This is my beast, ni muda kidogo toka nimemuweka pamoja ila hajawahi niangusha.
Motherboard natumia kama yako Gigabyte Z97, CPU ni i7-4790, 8GB Kingston Hyperx Fury, 1TB Western Digital HDD, 256GB Samsung 850-EVO SSD, hiyo display nilinunua cheaper kutoka kwa wachina 27" 2560x1440, GPU kwa sasa natumia GTX 1070 hii inapush QHD fps za kutosha, kama Overwatch haishuki 90FPS kwa Ultra Settings. Cover ni Corsair Obsidian series, feni sikununua extra, hizo zinawaka hapo zilikuja na cover sioni haja ya kununua nyingine coz sina hata mpango wa ku~overclock, it works smoothly. Imebaki kuvuta tu Oculus Rift nimalize na Virtual Reality moja kwa moja.

View attachment 390403
Mashine ya ukweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom