WAPENZI WA AFRO TZ TUKUTANE HAPA

WAPENZI WA AFRO TZ TUKUTANE HAPA

Septem

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2018
Posts
313
Reaction score
404
Kwa wapenzi wa muziki wa dansi, uwe wa kitanzania(kama vile 'zilipendwa' au za sasa kama vile zao wanatwanga, stono musica, au 'timu ya taifa'), kikongo(rhumba na soukous) tuna uhaba mkubwa wa vipindi vya TV na radio vinavyopiga nyimbo hizi. Zipo radio chache zimeweka vipindi maalum kwa ajili ya muziki huu wa dansi. Mojawapo ni Radio One. Kipindi hichi kinaongozwa nae Rajab Zomboko. Kipindi hiki kiitwacho Afro Tz;Mwendo kasi ni muafaka kwetu wadau wa muziki huu, hasa dansi ya 'nyumbani'. Kunakua na interviews na wadau mbalimbali wa dansi, nyimbo zote husikika hapa. Mimi ni ndau wa kipindi hiki kila jumatatu hadi alhamisi saa 4 hadi 7 usiku, 'sikosi'. Uzi huu ni maalumu kwetu wadau wa muziki huu wa dansi, tuwe tunajumuika kupeana habari na maujuzi mbalimbali juu ya muziki huu. Karibuni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom