Nani, Pius Ikongo? Ninyi mnaomjadili hapa Ikongo mnamfahamu? Huyu siyo Askofu, wala ushirika wa Wachungaji anaosema, wala haupo, wala hana Kanisa. Huyu ni kibaraka wa TISS ambaye kazi yake ni kuleta fitina kwa Wapentekoste. Alianza kazi yake ya kuleta fitina kwa Wapentekoste miezi kadha iliyopita, baada ya tamko kali la Tanzania Christian Forum (TCF), inayowajumuisha TEC ya Wakatoliki, CCT ya Waprotestanti, na PCT ya Wapentekoste. Tamko kali la TCF lilitolewa baada ya kuchomwa Makanisa mfululizo, na lilikuwa mwiba mkali kwa Serikali. Ndipo kibaraka Ikongo akatumwa kuleta fitina kwa Wapentekoste, na kusema kwa nini Viongozi wao wamekubali kushirikiana na waabudu sanamu. Akafukuzwa kwa aibu, kwenye kikao cha Wapentekoste pale Ubungo baada ya kuingia bila kuwa mjumbe, na kuleta fujo. Majuzi baada ya kifo cha Askofu Mkuu Kulola, aliibuka na kusema eti kabla ya kufa, Kulola alimwagiza aachane na huduma zake ndogondogo na kujiunga na EAGT. Ndipo akatangaza kwamba eti amejivua uaskofu wa huduma yake na kujiunga na EAGT na kuwa mshirika wa kawaida, kule Kigamboni. Leo, huyu mshirika wa kawaida, anajiita tena ni Askofu. Kwa ufupi, huyu ni kibaraka wa TISS ambaye kazi yake ni kuvuta mkwanja kwa fitina zake kwa Wapentekoste. Baada ya majina ya PCT kutupwa kapuni, na wakatoa malalamiko, ndipo Ikulu wakasema uongo kwamba majina hayakupelekwa, na wakaanza kumtumia tena Ikongo kuleta fitina eti Viongozi wa Wapentekoste wajiuzulu kwa kushindwa kupeleka majina. Ukweli ni kwamba majina yalipelekwa, Maaskofu wa PCT wasingeweza kuitisha Press Conference kulalamika wakati majina hayajapelekwa. Kutokana na fitina zake, Ikongo alipewa zawadi binafsi ya kuchagua mtu wa kumpeleka Bunge Maalum la Katiba. Akamchagua mtu wake, Respa Adam Miguna, anayesali EAGT Kigamboni, ambaye amewekwa katika orodha ya wajumbe wa kundi la Taasisi za Kidini, kama mtu binafsi, na Ikulu imesema eti PCT imtumie huyo huko Dodoma! Kwa taarifa ya JF, Respa hajaenda Dodoma mpaka leo, amejifungua kwa operesheni, siku chache zilizopita, na bado ni dhaifu. HIYO NDIYO TANZANIA!!!!