Wapendwa wa udom: Bima ya afya hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapendwa wa udom: Bima ya afya hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MAKOLE, Sep 6, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wapendwa, huu ni muendelezo wa post yangu ya (Ushauri wa Bure kwa waendao UDOM) pamoja na ile ya (wewe wa UDOM soma hapa fasta).
  Kwa umuhimu wake, nimeona nizitenge ili zipate kuonekana, pamoja na hizo mbili, natoa hii ihusuyo bima ya Afya. Utaratibu wa kujiunga na Bima ya afya tembeleeni link ya MFUKO WA AFYA (BIMA YA AFYA) katika link hii ifuatayo:

  Huduma kwa Wanachuo, hapo utapata kila kitu. Naomba ADMINS msiichanganye post hii kwa sababu ya umuhimu wake, huu ni utaratibu mpya hapa UDOM na pia haufahamiki kwa walio wengi.
   
 2. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huduma kwa Wanachuo


  Utangulizi.
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya pia unasimamia huduma za matibabu kwa Wanafunziwa Vyuo vya Elimu ya juu nchini kote. Utaratibu huu unalenga kuwapa Bima ya Afya wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu popote nchini ambapo mwanafunzi atapata huduma za matibabu wakati atakapokuwa masomoni na wakati wa likizo katika muhula husika.Huduma za matibabu kwa wanafunzi zinapatikana katika Hospitali,Vituo vya Afya, Zahanati na Maduka ya Dawa yaliyosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Tanzania.
  Utaratibu wa Kujiunga.


  • Wanafunzi wanaandikishwa chini ya udhaimi wa chuo husika kama Taasisi.
  • Kutakuwa na Mkataba maalumu wa maridhiano kati ya Taasisi husika(Chuo) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  • Mkataba kati ya mwanafuni na NHIF ni wa kipindi cha miaka mitatu , ambao unarejewa kila mwaka.
  • Huduma za matibabu kwa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu hazihusishi wenza wao wala wategemezi.

  Michango.


  • Chini ya utaratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, mwanafunzi husika anatakiwa kuchangia Shs 4,200 kwa Mwezi sawa na Shs 50,400 kwa Mwaka.
  • Wanafunzi ambao tayari wana vitambulisho vya matibabu vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, hawatahusika na uchangiaji huu kwa kuwa wao tayari ni wanachama wa Mfuko.
  • Taasisi husika (Chuo) ndiyo yenye dhamana ya kuwasilisha michango ya wanafunzi watakaoandikishwa chini ya utaratibu huu.
  • Michango ya kila mwezi ya wanufaika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya inatakiwa kuwasilishwa katika Ofi si za Kanda zilizopo karibu.
  • Jinsi ya Kujisajili.
  • Mwanafunzi atajaza fomu ya kujisajili,
  • Atatakiwa kuleta picha mbili za ukubwa wa pasipoti
  • Mwanafunzi atapata kitambulisho cha matibabu ambacho atakitumia kwa ajili ya matibabu.

  Mafao yanayotolewa

  Wanafunzi wa Vyuo vya ELimu ya Juu waliojiunga na NHIF watanufaika na mafao yote KUMI na MOJA yanayotolewa na Mfuko.
  Ikumbukwe kuwa mwanafunzi akishamaliza masomo anawajibika kurejesha kitambulisho cha matibabu cha NHIF kwenye chuo alikojiandikisha

  chanzo: http://www.nhif.or.tz. au link hii http://www.nhif.or.tz/index.php/huduma-kwa-wanachuo
   
 3. s

  sasha sarah Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  heello;;;so ukiwa umesha jisajini na nhif no need of paiyng medicall'''thn help me how can i registtn;;;
   
 4. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ndio hivyo, utakuwa ni mwanachama wa mfuko tayari, huna haja ya kusajili tena
   
 5. c

  chalema06 Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  xomkuu kuna pesa ya matibabu takribani laki moja tunalipa aple chuo, xo hiyo ndo wata i compaset kwenyemfuko au tunatakiwa kulipa tena elfu hamsini nyingine ukiachana na ile laki moja?
   
 6. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  kwanza nashukuru kwa taarifa hizi, naomba kuuliza yafuatayo
  1) Ile 100,000 ya medical capitation hatulipi??
  2) kujisajili na NHIF mpaka upate udhamini toka chuo wakati wamesema tuende tumejisajili na baadhi yetu sisi wazazi wote ni wakilima, tutafanyaje hapo??
  3) itakuaje tukishindwa kujisajili na NHIF??
  4) kwanini mpaka sasa UDOM hawajatoa admission latters?
  ni hayo tu
   
 7. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ingawa sina uhakika sana, ila msema kweli atakuwa ni joining instr. Kwa taarifa nlizonazo, wamesema soon watafungua ALIS ili kupata joining. Kama sijakosea sana, kama chuo kimeingia mkataba na mfuko wa bima, basi hiyo laki moja sasa haitalipwa, kwa sababu mwanzo wanachuo wote walilazimika kulipa hiyo pesa kwa madai kuwa chuo hakikuwa na mkataba na bima ya afya, hata hivyo hili ni jambo jema kwani litawasaidia. Jambo la kufanya ni kusubiria joining instruction. Udhamini wa chuo nadhani ni pale tu unapokuwa umesajiliwa na kupata namba ya usajili unakuwa ni mwanachuo halali wa na unazosifa za kudhaminiwa. Hata hivyo, sijajua itakuwaje ukishindwa kulipa kwani sijajua ni mechanism zipi zitatumika kulipa hiyo pesa, yawezekana wakasema ulipe za mwaka mzima pale mwanzo wa kila semesta. Kwa maelezo zaidi waweza wasiliana na bima watakueleza vizuri.
   
 8. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kwa maelezo ya bima ya afya ni kwamba badala ya laki moja cuo, lipa elfu 50, ya bima kupitia acount ya direct cost, chuo ndop kitapeleka bima ya afya
   
 9. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ndio inavyoonekana, hata hivo subirini maelezo ya chuo kupitia joining instr.
   
Loading...