Power G
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,884
- 1,200
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Katiba wamependekeza kuongezwa muda wa rais kukaa madarakani kutoka miaka mitano ya sasa hadi saba katika kipindi kimoja.
Wajumbe hao wanadaiwa kutoa wazo hilo ndani ya Kamati Namba 12 ilipokuwa ikijadili sura ya saba ya Rasimu ya Katiba, inayohusu Serikali, Rais, Makamu wa Rais na Baraza la Mawaziri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Paul Kimiti, wazo la kutaka kuongezwa kwa muda huo lilijengwa katika msingi kwamba miaka saba itamwezesha kiongozi huyo mkuu wa nchi kutekeleza vyema ahadi alizotoa kwenye uchaguzi.
Ni mtazamo wa baadhi ya wajumbe kuwa pamoja na hilo kuongeza miaka kutaepusha utumiaji wa fedha nyingi ndani ya muda mfupi kutokana na gharama za uchaguzi, kilisema chanzo chetu ndani ya kamati.
Waliona kwa nchi zenye uchumi mchanga, suala la kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano linagharimu ukuaji katika sekta ya maendeleo kutokana na gharama kubwa za uchaguzi huo.
Kimiti alisema licha ya hoja hiyo kuwa na mashiko, wajumbe walisema ikiwa muda wa kukaa madarakani utaongezwa, hauwezi kuwa kwa rais pekee, bali kwa wabunge na nafasi nyingine kama madiwani.
Source: Mwananchi .
Maoni yangu:- Hiyo ndiyo CCM yenye kutuletea katiba mpya watz!!