Wapenda matanuzi presha zinapanda, waadilifu hawana wasiwasi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,611
Wenye vyeo serikalini wanaweza kugawanywa katika makundi mawili, wale wenye kupenda maisha ya kifahari na wale waadilifu wenye kujua maana ya neno "kiasi".

Wale walioendekeza maisha ya matanuzi, yenye kupenda safari zisizokuwa na ulazima wakati wa awamu ya tatu na ya nne, sasa hivi hawana amani akilini, wakisikia gari inapoga honi nje wanajua ndio tayari saa mbaya maishani imeshawadia.

Wale wenye kuziona nyumba za bei mbaya za kina Tom Cruise na Bilii Gates wakati wanatazaa tovuti na magazeti yanayohusiana na maisha ya wamarekani halafu wakafanya kila njia mpaka wajenge copy za nyumba hizo kwenye viwanja vyao vya mbezi beach na salasala kwa kutumia fedha iliyokusudiwa kuyatatua matatizo ya maskini wa nchi hii, sasa hivi wakiona namba ambayo hawajaisave kwenye simu zao presha inapanda, hawana amani ya kuipokea.

Wale ambao wenye kuliona gari la milioni 300 kwenye tovuti za magari halafu wakahakikisha wanalliendesha kwenye barabara zetu, lakini wakilinunua kwa kutumia fedha za michongo ya serikali, leo hii hawana amani moyoni, wanajua muda wowote ule kitanuka.

Lakini wale waadilifu ambao wamejenga nyumba zao kwa kutegemea fedha inayoelezeka vizuri hawana hofu yoyote ile.

Wale ambao wanasomesha watoto wao kwa kutumia fedha ambayo ni jasho lao, wakipigiwa simu hata kama namba hawajaisave, wala hawana presha ya kupokea.

Wale ambao walikuwa na mafungu makubwa ya fedha ambayo matumizi yake yapo chini ya maamuzi yao halafu wakazielekeza zinapotakiwa kutumika bila ya wao kugusa hata thumni, leo hii hawana haja ya kulala usingizi wa hofu kama vile mtu amelala kwenye kituo cha treni, yaani akisikia honi tu anaamka na kuanza kubeba mabegi kwa ajili ya safari.

Muadilifu na mwema ni watu wawili ambao hawawezi kugundulika kwa kuzitazama sura zao. Ukiwakuta misikitini wanakuwa na sura za upendo wa hali ya juu, ukiwakuta makanisani, ndio wanaokuwa wanapitisha kapu la sadaka na mwisho huzipeleka mbele kwa padre ili waumini waweze kupata baraka ya pamoja.

Matendo yao wanapokuwa wamekabidhiwa mali ya umma yenye thamani kubwa, ndiyo siku zote huwatofautisha.
 
Hivyo wako hao unaowasema? Au Magufuli itambidi a-overlook makosa madogo madogo. Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom