Wapanga kuvuruga ziara ya Ki-moon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapanga kuvuruga ziara ya Ki-moon

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Feb 25, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Serikali imebaini kuwapo mpango mchafu wa kutaka kuvuruga ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon nchini, imeelezwa.Akizungumza jana Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema kuna kundi la watu wanaojiita 'Wazee wa Pemba' linapanga siku hiyo kuingilia ratiba ya mgeni huyo na kufanya maandamano.

  Katibu Mkuu wa UN anatarajia kufanya ziara kuanzia kesho hadi Jumamosi, kutokana na mwaliko aliopewa na Rais Jakaya Kikwete walipokutana New York, Marekani, Septemba mwaka jana.

  Waziri alisema baada ya Serikali kulibaini hilo, hivi sasa inalifanyia kazi ikiwa ni pamoja na lile la wapinzani wa Ba Ki-moon kutoka nje ya nchi, wanaopanga kutumia baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari mbaya kumhusu."Ombi letu ni kuhakikisha watu hao hawafanikiwi katika azma yao ya kutumia vyombo vya habari vya hapa nchini kuandika mambo mabaya ya kumchafulia jina mgeni wetu," alisema Waziri Membe.

  Waziri alisema ziara ya Ban Ki-moon ina lengo kuu moja, la kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na UN. Katibu Mkuu akiwa nchini mbali ya kufanya mazungumzo na Raia Kikwete, pia atatembelea miradi inayosimamiwa na mashirika mbalimbali ya UN na mradi wa majaribio wa ONE UN.

  Pia atakwenda Zanzibar keshokutwa na kufanya mazungumzo na Rais Amani Abeid Karume na kuzindua jengo la UN Zanzibar, kisha atakwenda Arusha kutembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Katibu Mkuu huyo aliipa heshima kubwa Tanzania ya kumteua Mtanzania kushika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk Asha-Rose Migiro, ambaye ni mwanamke wa kwanza duniani kushika wadhifa huo.

  Waziri Membe alisema Ki-moon ni rafiki mkubwa wa Tanzania na Afrika, kwani hata kabla ya kuwa na nafasi aliyo nayo sasa, akiwa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, aliishawishi serikali yake kuipa Tanzania misaada. Miongoni mwa misaada hiyo ni kujenga daraja la Malagarasi, Kigoma, ujenzi wa vyuo vya ufundi, ujenzi wa hospitali ya kufundishia chuo kikuu Muhimbili na mingine mingi.

  Alitoa mwito kwa wananchi kumpokea kwa wingi na kwa heshima kubwa. Mei 12 mwaka jana wazee 12 walikamatwa na Polisi Zanzibar kwa tuhuma za kudai Pemba ijitenge na Zanzibar, kwa madai kuwa ilikuwa imesahaulika kwa maendeleo. Kwa mujibu wa ofisa usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), aliyetajwa kwa jina la Said Miraji, wazee hao walikamatwa usiku.

  Wazee hao wiki moja kabla walikuwa wamewasilisha madai yao kwa Ofisa Mwandamizi wa UN, Dar es Salaam, Oscar Fernandez-Taranco, wakimtaka awasilishe madai yao hayo kwa Ki-moon.Baada ya kukamatwa kwa wazee hao, CUF ilisema ilikuwa imewaagiza wabunge wake kutunza familia za wazee hao, huku chama hicho kikishughulikia hatima yao.

  Miraji alithibitisha kuwa waliokamatwa walikuwa wafuasi wa CUF. Mwezi mmoja kabla ya kukamatwa kwao, wazee hao walikuwa wamemtaka aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Mark Green, kuwasilisha ujumbe wao kwa Rais George Bush, ili awasaidie kujitenga na Muungano wa Zanzibar na Bara.

  SOURCE:Habari leo.

  Duh hii kali.Membe anataka kutuaminisha wazee wapemba wanataka kuvuruga ziara ya Ki-moon,hawana hoja ya msingi.Kwa maoni yangu naamini wazee wa Pemba wanataka kuwasilisha malalamiko ya mauaji ya ndugu zao wakati wa uchaguzi mkuu 1995.Serekali kwa upande wake wanaona hizo ni vurugu hawataki jumuiya ya kimataifa na hasa katibu mkuu kujua maafa yaliyowakuta ndugu zetu wa Pemba.Chonde chonde Membe wazee wa kipemba wapewe nafasi ya kuwasilisha malalamiko pengine wahusika wakuu wa mauaji wataweza kufikishwa mahakamani.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama wanataka kuwasilisha madai yao ndio kuvuruga ziara? naona Membe anataka kukuza mambo
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nimeisoma habari yaonekana waziri ni mtu wakupenda kutia chumvi mambo. jamani hivi huyu ana background yoyote na diplomasia au ndo ushkaji???

  jamaa anatulet down sana kwani anga za kimataifa tulijulikana kama watu makini kwa sera yetu na viongozi wetu ila membe binafsi ananikera.

  vipi mkuu anamwamini sana siyooo na labda keshampa signal jiandae mwanaaaa.....
  alianzia kuchemka sulivan summit, tamko la zimbabwe.......... OIC!!!!!!
  VIPI HUYUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa naona serikali inataka ujipatie kaujiko flani eti wamegundua wanao taka kuvuruga ziala ya katibu mkuu wa UN ambacho si kitu cha kweli wanatudanganya tu hawa hakuna kitu kama hicho mbona mbinu chafu za mafisadi hawazioni??????
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  TZ zikianza kauli kama hizo usishangae kama kutatokea kamata kamata ya Polisi ama imeshatokea. Unaweza kuta saa hizi wale wazee wako ndani, ama watazuiwa wasitoe mguu Pemba.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wapemba hao, tahadhali lazima ichukuliwe..
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hili linawezekana kabisa, kauli hizi ni dalili za kuandaa kamatakatmata zisizo na msingi
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Aaaagh!!!!

  Ngongo na wengine wengi; tuwe makini sasa naona huu upinzani unatufanya tunakuwa na vimini vya akili au u-bikini wa fikra... Kilichotolewa ni tahadhari!! na wapemba wanataka fikisha hoja yao, sasa solution ni kulala barabarani? si waende kwa UN rep, vituo vya habari n.k.

  Mimi sijanywa maji ya bendera lakini baadhi ya mbinu tunazopanga ni za zama za kale za mawe;

  Nakumbuka wale wa London waliopigia kelele mwenge wa olympic, wamepata nini???

  HIZO KAMATA NI ZA LAZIMA IWAPO MTU ANAONESHA DALILI MBAYA, HATA MAKWETU KUNA WAKATI AKIJA MGENI WA BABA NA IKAONEKAKA KIJANA UMELEWA AU HAUKO SAWA UNAWEKWA CHUMBANI HADI WAGENI WAONDOKE....

  WATANZANIA TUAMKE, HIZI DRAMA ZA MEDIA ZIPO TUUU
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Acha Lugha za kibaguzi.

  Nimemsikia Dr.Mahiga akisema kuwa mwakilishi wa UN mkaazi ,amezungumza nao na ameshamalizana na wazee hao na hivyo hakuna tishio lolote linaloweza kujitokeza .

  Membe alitaka kuongeza hofu na ama alitaka kufunika kombe ili hata wakijitokeza na madai yao ya msingi basi polisi watakapowashambulia kwa mabomu basi vyombo vya kimataifa viandike kuwa walitaka kuvuruga ziara ya Moon.

  Watawala wetu ni wataalamu sana wa propaganda , ila bado wapo kwenye propaganda nyeusi mpaka nyakati hizi .
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mwakilishi UN awatuliza Wapemba kuhusu ziara ya Ban Ki-moon
  Elias Msuya na Levina Jackob

  MWAKILISHI mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Oscar Fernandez Taranco, amesema kwamba, hakutakuwa na tishio lolote la kuvurugwa kwa ziara ya siku mbili ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayoanza leo.


  Taranco ametoa taarifa hiyo siku moja tu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kudai kuwa kuna makundi yaliyojipanga kuvuruga ziara hiyo, akilitaja kundi la watu wanaojiita, "Wazee wa Pemba" na la wapinzani wa katibu huyo, ambaye ni raia wa Korea Kusini kuwa ndiyo yenye mpango huo.


  Wazee wa Pemba wanataka Umoja wa Mataifa uwasaidie ili kisiwa hicho kijitenge na Zanzibar ili kiwe na uhuru kamili, wakidai kuwa, kisiwa hicho kimekuwa kikibaguliwa katika mipango ya maendeleo na Membe alidai wazee hao walitaka kuandamana ili kuivuruga ziara hiyo.


  Alisema kuwa, Wapemba hao pamoja na kundi jingine kutoka nje ya nchi walipanga kufanya maandamano ya kumkashifu Ban Ki-moon na kusoma risala ya matatizo yao endapo wangefanikiwa kuusimamisha msafara wake.


  Lakini Taranco aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, ameshaongea na kundi hilo baada ya kupokea barua ya malalamiko yao waliyoyawasilisha ofisi za Umoja wa Mataifa nchini.


  “Ni kweli tunalijua tatizo hilo na kwa bahati nzuri hao viongozi wa Wapemba nimekutana nao leo asubuhi na wamenieleza matatizo yao tukaongea na tumekubaliana kuyamaliza,” alisema Taranco, ambaye hata hivyo hakufafanua kuwa UN itamaliza lini madai ya Wapemba hao.


  “Malalamiko ya Wapemba tumeshayajadili sana na nilishayawakilisha Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na juhudi zinafanyika ili kuyamaliza. Hivyo nawahakikishia Watanzania kuwa, hakutakuwa na tishio lolote katika ziara ya katibu mkuu huyo.”


  Hii ni mara ya kwanza kwa Ban Ki-moon kufanya ziara nchini tangu achaguliwe kushika wadhifa huo mkubwa kwenye umoja huo wenye nguvu duniani. Ziara hiyo inaanza leo na kumalizika kesho wakati raia huyo wa Korea Kusini atakaposhiriki katika shughuli mbalimbali katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha.


  Akiwa Tanzania, Ban atafanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete kuhusu migogoro inayolisumbua Bara la Afrika na jukumu la kulinda amani barani humo.


  Katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira, katibu huyo wa UN atapaa kwa ndege juu ya Mlima Kilimanjaro ili kushuhudia athari za ongezeko la joto duniani.


  Ban amefurahishwa na maendeleo ya Tanzania katika kutekeleza malengo ya milenia, ikiwa ni pamoja na kupambana na umaskini. Lengo la ziara yake barani Afrika ni kuhimiza viongozi kutumia ipasavyo rasilimali na misaada kwa ajili ya kutekeleza malengo ya milenia.


  Nchi nyingine atakazotembelea ni Misri, Afrika Kusini, Congo, Rwanda, Nigeria na Senegal.

  Source:Mwananchi
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kama ni kufanya maandamano tu ni jambo linalokubalika kisheria. Na kama ni kusoma risala hata kama ya kukashfu umja wa mataifa ni haki kisheria. UN sasa hivi ni useless kwa helpless people. Lakin inatumia hao hao kujinadi duniani, naona hao wapemba wana maana nzuri tu. Kama hakunadalili ya kufanya vurugu waache waandamane tu.
   
Loading...