Wapanga kumng'oa Mbunge Lema

Wapanga kumng'oa Mbunge Lema

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
SIKU chache kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu wa- Rais, wabunge na madiwani, hali si shwari kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Bw. Goodbless Lema (CHADEMA), kutokana na baadhi ya makada, wanachama wa chama hicho, kufanya kampeni za kutaka kumng'oa mbunge huyo.

Kampeni hizo zinadaiwa kufanywa na makada hao kimyakimya wakitumia mwamvuli wa chama kuhakikisha Bw. Lema anaanguka katika uchaguzi huo kama chama chake kitampitisha kuwania nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza na vyombo vya habari jana kwa niaba ya Bw. Lema, Katibu wake Bw. Inocent Kisayange, alisema kundi hilo limefanikiwa kukusanya makada wengine na kuwashawishi waungane kumkataa mbunge huyo ili asiweze kupita.

Alisema baadhi ya makada hao wamefukuzwa uanachama na wengine walijifuta wenyewe kutokana na makosa waliyofanya ambao wameungana na wenzao kutoka Arumeru Mashariki na Igunga ili kumchafua Bw. Lema aweze kukosa ubunge kwa madai mbunge huyo hajafanya lolote tangu achaguliwe.

Aliongeza kuwa, makada hao wanatumia mbinu mbalimbali kuwakusanya wananchi na kuwaambia wao ni viongozi katika sekretarieti ya chama na kumchafua mbunge huyo.

"Tumefanya uchunguzi wa kutosha na kugundua nyuma ya hawa vijana yupo kada mmoja wa CCM anayetaka kuwania ubunge wa jimbo hili hivyo anawawezesha hawa vijana ili wafanye mikutano na kumchafua Bw. Lema," alisema.

Bw. Kisayange alisema, katika kundi hilo ambalo limejikita zaidi kufanya kampeni za kukiharibia chama hicho, limekuwa likitumia mbinu za kutaka kuwasaidia wanawake na vijana kwa kuwapa mikopo jambo ambalo si kweli.

Alisema tayari ofisi ya mbunge imeshajipanga kupambana na kundi ambalo limeamua kuasi chama kwa ajili ya maslahi binafsi na kusambaza habari za uongo dhidi ya Bw. Lema.


Chanzo: Majira Gazeti
 
Kwanu makada ndio wanao piga kura? Yeye alichaguliwa na wana wa arusha na atachaguliwa na wana wa arusha
 
Makada hawana wingi kiasi cha kuwazidi wakaazi wa arusha
 
Ndoto hutokana na fikra nyingi za mchana ama msongo wa mawazo, hamzuiwi kuota na mnaposimulia mnaonyesha jinsi mnavyoweweseka.
 
Badala ya kupambana jinsi ya kuinua uchumi wa nchi bise kungoa mbunge kweli watanzania tuna safari ndefu ya kujikomboa
 
  • Thanks
Reactions: 999
Nimesikia kwa kuuliza wananchi wakiwemo wanachadema,wameniambia lema hafai na hajafanya maendeleo arusha.mnalijua hilo?.
 
Hata kwenye kura za maoni amepigwa mwereka,, Hakubaliki kabisa haelewani mpaka na Golugwa,Nanyaro undugu wake na Mbowe unampa kiburi
 
Mmmh!hao watu uliowauliza wanaishi sehemu gani? hapa arusha ya lema.
 
Lema is lacking independent thinking...wapigakura wa Arusha tulikosea sana
 
nimesikia kwa kuuliza wananchi wakiwemo wanachadema,wameniambia lema hafai na hajafanya maendeleo arusha.mnalijua hilo?.
ni kweli lema hatakiwi kwenye kikao cha siri cha ccm kupanga jinsi kuiba kura ar mjini.
 
Back
Top Bottom