Wapalestina wanatumika kisiasa?

Wapalestina wanatumika kisiasa?

Shinoga

Member
Joined
Dec 8, 2012
Posts
16
Reaction score
4
Huwa najiuliza hivi ni kwa nini wapalestina(waarabu) walikataa azimio la umoja wa mataifa la 1948 lililogawa 'palestina' kuwa mataifa mawili (israel ya wayahudi na palestina ya waarabu)? Nikiangalia ramani ya partitioning ile naona wapalestina walifanya makosa makubwa sana kukataa azimio lile, kwani liliwapa eneo sawa na Israel , au pengine kubwa zaidi ya israel. Nashindwa kuelewa kwa nini wapalestina mwaka jana mwishoni walikuwa wanashangilia azimio la baraza kuu la UN juu ya kutambuliwa taifa la palestina kwenye eneo dogo la Gaza na West bank (lenye makazi mengi ya wayahudi) wakati zaidi ya miaka 60 iliyopita walikataa azimio lililowapa eneo kubwa kwa ajili ya taifa lao?

JIBU linalonijia ni kwamba wapalestina wanatumiwa na waarabu wenzao kisiasa katika kuendeleza uhasama wao na wayahudi. Haiwezekana Misri, Jordan zi-negotiate kurudishiwa maeneo yao yaliyotekwa na Israel wakati wa vita (iliyoanzishwa na waarabu), halafu hao hao wawashawishi au wawachochee wapalestina wakatae muafaka na Israel.
 

Attachments

  • palestine.JPG
    palestine.JPG
    36.2 KB · Views: 86
Back
Top Bottom