Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,188
- 10,668
Ujumbe wa Palestina katika Umoja wa Mataifa umeandaa rasimu ya azimio jipya la kulaani hatua ya utawala haramu wa Israel kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.
Kanali ya televisheni ya Press TV ya Iran imelinukuu gazeti la kizayuni la Haaretz ambalo limesema kuwa, tayari wawakilishi hao wa Wapalestrina katika Umoja wa Mataifa wameanza kusambaza nakala za rasimu hiyo kwa nchi wanachama wa UN. Aidha imearifiwa kuwa ujumbe huo unafanya mazungumzo na baadhi ya nchi za Kiarabu kuhusu rasimu ya azimio hilo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Habari zinasema kuwa, rasimu hiyo inafanana na iliyoandaliwa Februari mwaka 2011, lakini ikaangushwa na Marekani kwa kutumia kura yake ya veto, licha ya nchi zingine 14 za Baraza la Usalama kuiunga mkono.
Kadhalika Hareetz imeripoti kuwa aghalabu Wapalestina wanazitaka nchi zote za Baraza la Usalama la UN kuunga mkono rasimu hiyo, wakati Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina atakapoenda mjini New York nchini Marekani Aprili 22.
Rasimu hiyo imamghadhabisha na kumtia kiwewe Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye amemtuhumu Abbas kuwa anahujumu juhudi za amani.